RAIS WA ZAMANI WA ALGERIA AFARIKI DUNIA


Rais wa zamani wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Bouteflika aliongoza nchi hiyo kwa karibu miongo miwili na kuachia madaraka mwaka 2019 baada ya jaribio lake la kugombea muhula wa tano kusababisha maandamano makubwa.

Alikuwa kiungo muhimu katika vita vya kupigania uhuru wa Algeria miaka ya 1950 na 60.

Mwaka 1999, baada ya Algeria kujikwamua kutoka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilisababisha vifo vya karibu watu 200,000, alikuwa raia baada ya kuombwa na jeshi la nchi hiyo.

Bouteflika hajaonekana hadharani tangu mwaka 2013, baada ya kuugua kiharusi ambacho kiliathiri uwezo wake wa kuzungumza na kutembea.

Chanzo - BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post