BARAZA LA VYAMA VYA SIASA KUJENGA SIASA SAFI ZISIZO NA CHUKI - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Friday, August 27, 2021

BARAZA LA VYAMA VYA SIASA KUJENGA SIASA SAFI ZISIZO NA CHUKI

Na Magrethy Katengu - Dar es salaam

Baraza la vyama vya siasa nchini  limesema litahakikisha Viongozi wote wa vyama vya siasa wanafanya siasa za kizalendo,amani, utulivu na kujenga democrasia kwa kizazi cha sasa na kijacho kisichokuwa na chuki.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi kamati za uongozi mbalimbali za baraza hilo, Mwenyekiti wa Baraza  la vyama vya siasa, Juma Khatibu amesema wanahitaji kujenga usawa wenye ,misingi ya demokrasia makini na  kuweka mbele zaidi uzalendo na si siasa za chuki ambazo hubomoa taifa.

"Kamati hizi tulizoziweka  zitahakikisha mpango mkakati ni kijenga Taifa la kizalendo lenye amani na utulivu huku siasa za kistaarabu zikifanyika kwa ustaarabu",aliaema Khatibu.

Aidha amesema wameunda kamati mbalimbali ikiwemo kamati ya fedha,maadili ,sheria ikiwa na matarajio ya kufanyakazi kwa pamoja na vya vyote bila ubaguzi katika kujenga Tanzania imara kiuchumi na kiplomasia.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages