MBOWE NA WENZAKE WAFIKISHWA MAHAKAMANI


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kukiwa na ulinzi mkali.

Washtakiwa hao wamefikishwa Mahakamani hapo saa leo Ijumaa, Agosti 6, 2021  wakiwa kwenye basi dogo la Magereza likisindikizwa na magari mawili ya wazi yenye askari magereza wenye silaha za moto.

Baada ya kuwasili washtakiwa wote walishuka na kuelekea kwenye mahabusu ya Mahakama.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Halfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Lingwenya.

Mbowe na wenzake wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama na kutenda kosa na kutoa fedha kwa ajili ya kufadhili shughuli za ugaidi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post