LEMBELI ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE USHETU

 Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Kahama mkoani Shinyanga, mwaka 2005 hadi 2015, James Daud Lembeli  amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuchaguliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mbunge wa jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga.


Akizungumza na waandishi wa habari leo muda mfupi baada ya kuchukua fomu hiyo katika ofisi za CCM wilaya ya Kahama, amesema kuwa endapo chama kitampa ridhaa ya kugombea ubunge wa jimbo hilo ataendeleza miradi yote ya maendeleo iliyoanzishwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Elias John Kwandikwa.

“Vipaumbele vyangu nitakavyoanza navyo  endapo chama changu kikinipa ridhaa ni kuboresha sekta ya elimu, afya, maji, umeme na miundombinu ya barabara ambayo mtangulizi wangu Elias Kwandikwa alivitekeleza kwa weledi,”amesema Lembeli.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments