JAMAA AJINYONGA BAADA YA KUACHWA NA MKEWE AKIWA NA WATOTO WATANO



Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Philemon Tandu (50) Mkazi wa kijiji cha Ng’wandakw kata ya Haydom wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara  amefariki dunia kwa kujinyonga baada ya kuachwa na mke wake akiwa na watoto watano.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara ACP Marrison Mwakyoma amesema tukio hilo limetokea juzi katika kijiji hicho ambapo Philemon Tandu  alijinyonga kwa kutumia kamba ya katani shingoni karibu na nyumba yake baada ya mkewe Christina Elia (45) kumuacha akiwa na watoto watano akisema hamtaki tena.

Kamanda Mwakyoma amesema chanzo cha kifo hicho ni matatizo ya familia kwani mara baada ya Tandu kuachwa na mkewe walijaribu kusuluhisha ugomvi wao ili wasiachane na walee watoto wao ila ikashindikana mwanamke huyo akaondoka.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments