IGP SIRRO AWATAKA CHADEMA WASUBIRI MAHAKAMA ITAKAVYOAMUA JUU YA MBOWE - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Monday, August 2, 2021

IGP SIRRO AWATAKA CHADEMA WASUBIRI MAHAKAMA ITAKAVYOAMUA JUU YA MBOWE

 

Na Dickson Billikwija,Dar es Salaam

Mkuu wa Jeshi la polisi nchini IGP SIMON SIRRO amekita Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA)kuacha maneno maneno na kusubiri maamuzi ya Mahakama itakavyootoa maamuzi kwa Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe.

Akiongea leo Agosti 02,2021 jijini Dar es Salaam mbele ya Wanahabari IGP Sirro alisema kufanya maandamano ni sawa na kuvunja sheria na ukivunja sheria ni sawa na kufanya uhairifu,

Alisema wafuasi wa CHADEMA wasimuone Mwenyekiti wao Kama malaika ni mtu ambaye hawezi kukosea,

Kwa msisitizo aliendelea kusema kwamba wao (CHADEMA) wamuulize Mwenyekiti wao Kama ameonewa na ana uhakika kama ana imani na dini yake atasema ukweli.

IGP Sirro aliwataka watanzania kutoshawishika na hao vyama Vya upinzani kwa kuwataka eti wafanye maandamano kuja dar na kwenda mpk Mahakama Kuu.

IGP Sirro alisema yeye kwa kushirikiana na jeshi la polisi hawata waacha waalifu.Alisema mwenye hekma aiachie Mahakama iamue.

Sanjari na hi]nlo IGP Sirro aliziomba halmashauri zote Nchi kutunga sheria ndogondogo zitakazosaidia wananchi kuchangia Ulinzi shirikishi,


Alizipongeza Halmashauri mbili za Temeke na Kinondoni kuwa na sheria ndogondogo ambazo zimekuwa mwongozo kwa jeshi la polisi

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages