Breaking

Post Top Ad

https://refpasrasw.world/L?tag=d_1066073m_7669c_&site=1066073&ad=7669

Friday, August 27, 2021

WAZALISHAJI WA BIDHAA NCHINI KUONGEZA UBORA WA BIDHAA ZAO

 

Na Magrethy Katengu Dar es salaam

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Visiwani Zanzibar Mhe. Omar Shaban ametoa Wito kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali kwenye Viwanda na Wafanyabiashara kutumia Falsafa ya kuongeza ubora wa mifumo endelevu ya Biashara zao inayojulikana kama KAIZEN.

Mhe. Omar Shaban ametoa wito huo wakati akifunga Kongamano la KAIZEN Brani Afrika lililofanyika kwa siku tatu jijini dar es salaam, ambalo limeshirikisha wadau kuhusu mafanikio na kubadilishana uzoefu ili kukuza viwanda kupitia harakati za kueneza falsafa hiyo.

Hata hivyo amesema viwanda vingi barani afrika vinakabiliwa na changamoto ya gharama kubwa za uzalishaji wa bidhaa, wafanyakazi kutokuwa na morali ya kufanya kazi hali inayosababisha bidhaa hizo kutopata soko la uhakika na kushindwa kuhimili ushindani.

Kongamano hilo limekuwa na Kauli mbiu isemayo Fursa za Kuharakisha Maendeleo ya Viwanda na Biashara Barani Afrika, ikisisitiza uongezaji ubora, tija na teknolojia za dijitali katika uzalishaji na undelezaji wa viwanda vidogo na biashara ili kukuza uchumi wa ndani. 

Kwa upande wake Mratibu wa Kongamano la KAIZEN, Idara ya Biashara na Viwanda Bi. Jane Liattu amesema kongamano hilo limetoa tuzo kwa viwanda mbalimbali vya Afrika vilivyofanya vizuri katika kutoa huduma zake na uzalishaji huku akisema hakuna kiwanda cha Tanzania kilichopatiwa tuzo akieleza kuwa hali hiyo haimaanishi kuwa viwanda vya Tanzania havijafanya vizuri.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages