WIKI YA MWANANCHI YAKAMILIKA ZANACO YA ZAMBIA IKIICHAPA YANGA SC 2-1 MBELE YA MAELFU YA MASHABIKI


Ikiwa leo ndo kilele cha wiki ya mwananchi kwa mashabiki wa klabu ya Yanga ambapo sherehe hiyo imefanyika Jijini Dar es Salaam wamecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Zanaco Fc ya nchini Zambia ambapo wamefungwa mabao 2-1 licha ya kipindi cha kwanza kuongoza.

Mchezo wa leo ulikuwa na ushindani mkubwa baada ya utambulisho wa wachezaji mbele ya mashabiki wengi waliojitokeza Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es salaam.

Alianza Heritier Makambo kupachika bao dakika ya 30 lilikuja kusawazishwa kipindi cha pili Hakim Mniba na lile la pili lilifungwa na Kelvin Kapumbu dk 77.

Kelvin Kaindu, Kocha Mkuu wa Zanaco amesema kuwa mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa wapinzani wao.

Kilele cha Wiki ya Mwananchi kulikuwa na matukio mengi ikiwa ni pamoja na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali kama Nandy, Mopao, Juma Nature na Temba ambao walitoa burudani za kutosha.

Sherehe hiyo ilihudhuliwa na baadhi ya viongozi wakubwa Serikalini akiwmo Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla ambaye alipata fursa kuzungumza na mashabiki katika hafla hiyo.

Mashabiki waliojitokeza walikuwa wengi na licha ya timu yao kupoteza bado waliwashangilia wachezaji wao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post