MUHOJA AZINDUA MAKAMBI ,AWATAKA WAUMINI KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA UVIKO - 19 | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, August 8, 2021

MUHOJA AZINDUA MAKAMBI ,AWATAKA WAUMINI KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA UVIKO - 19

  Malunde       Sunday, August 8, 2021
Meneja wa makambi Usharika wa Ndembezi unao jumuisha makanisa manne ya Ngokolo, Ibadakuli, Bugweto na Ndembezi Deusi Muhoja akizindua makambi hayo yatakayodumu kwa muda wa siku 7.

******
Meneja wa makambi Usharika wa Ndembezi unao jumuisha makanisa manne ya Ngokolo, Ibadakuli, Bugweto na Ndembezi Deusi Muhoja amezindua makambi hayo yatakayo dumu kwa muda wa siku 7.

Akizindua makambi hayo,Muhoja amewaasa waumini wa kanisa la Waadventista Wasabato na waumini wa Madhehebu mengine
kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa UVIKO 19 kwa kufuata maelekezo na ushauri una tolewa na wataalamu wa Idara ya afya mkoani humo

Muhoja ambaye pia ni Afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ametoa wito huo Agosti 7, 2021 katika hafla fupi ya uzinduzi wa makambi ya waumini wa Kanisa la waadventista Wasabato yatakayodumu kwa muda wa siku 7 yakihudhuria na viongozi pamoja na waumini wa kanisa la wasabato kutoka katika makanisa manne yanayounda usharika huo.

Amesema ni wajibu wa waumini kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa UVIKO 19 pamoja na kuendelea kumuomba
Mungu ili aweze kusaidia kuliepusha taifa na janga hilo.

Muhoja ametoa wito kwa madhehebu ya dini mengine hapa nchini kushirikiana na serikali katika katika jitihada za kupambana na janga hilo kwa kuchukua tahadhari na kumuomba Mungu.

Muhoja amewataka waumini wakanisa hilo kuhakikisha wanavaa barakoa pamoja na kuhakikisha wananawa mikono kwa maji safi tiririka na sabuni kabla ya kuingia katika maeneo ya kanisa hilo.

Kwa upande wao baadhi ya waumini wa kanisa la Waadventista Wasabato Ndembezi wameahidi kuzingatia maelekezo na utaratibu unaotolewa na viongozi wa kanisa katika kuhakikisha waumini pamoja na wananchi wanashiriki makambi kwa kuchukua taadhari dhidi ya ugonjwa wa UVIKO -19
Meneja wa makambi Usharika wa Ndembezi unao jumuisha makanisa manne ya Ngokolo, Ibadakuli, Bugweto na Ndembezi Deusi Muhoja akizindua makambi hayo yatakayo dumu kwa muda wa siku 7.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post