IMAMU MKUU SHEHE SHARUBUTU ACHANGIA MAMILIONI YA FEDHA KUSAIDIA UJENZI WA KANISA LENYE UTATA


Imamu mkuu wa Ghana, Shehe Osman Sharubutu amechangia zaidi ya $8,000 (£5,800) sawa na Shilingi Milioni 18.4 za Tanzania ili kusaidia ujenzi wa kanisa kuu la kitaifa lenye utata.

Ghana ina historia ya kuwa na mahusiano mazuri ya amani ingawa hatua ya kiongozi wa dini kuchangia fedha nyingi kwa imani nyingine si jambo la kawaida.

Imamu mwenye umri wa miaka 102-amesema ameamua kufanya jambo hilo ili kuimarisha amani ambayo ipo kati ya wakristo na waislamu.

Kiongozi huyo wa kiislamu ambao ni wachache nchini Ghana, amesisitiza kuwa anataka kuhakikisha kuwa heshima yake ni amani.
Miaka miwili iliyopita kiongozi huyo alihudhulia ibada ya Pasaka katika kanisa katoliki na kusababisha gumzo kwenye mitandao ya kijamii.
Licha ya wengi kukasirishwa na kitendo chake cha kushiriki katika misa kusali Shehe Sharubutu alisisitiza kuwa alikuwa anabudu hapo anaimarisha uhusiano wa kati ya waislamu na wakristo.

Na msemaji wake alisema "Chifu mkuu anabadili mtazamo juu ya dini ya kiislamu kuwa y amigogoro, chuki kwa wengine bali ni deni yenye upendo , amani na inasamehe."

Na sasa serikali imezindua ujenzi wa kanisa na kuwasisitiza Waghana wachangie katika ujenzi huo.

Kanisa hilo linajengwa katika mji mkuu wa Accra, na gharama za ujenzi zinatarajiwa kuwa zaidi ya dola milioni 100.

Ujenzi wa kanisa la taifa unatarajiwa kumalizika mwaka 2024, ikijumuisha na makumbusho ya biblia na ukumbi unaoenea viti 5,000.

Ingawa itakuwa na ufadhili binafsi , lakini wengi wamekosoa mradi huo na kuelezea kuwa ujenzi wa kanisa hilo si kipaumbele kwa sasa ambako kuna mabadiliko ya kiuchumi.

Chanzo - BBC Swahili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments