Tanzia : MTANGAZAJI MAARUFU JUMA AHMED BARAGAZA 'JB' AFARIKI DUNIA

 Mtangazaji maarufu wa Radio Free Africa na Star TV jijini Mwanza Juma Ahmed Baragaza (JB) amefariki dunia leo Jumamosi Agosti 7, 2021 baada ya kuugua ghafla mkoani Morogoro.

 JB Atakumbukwa zaidi katika vipindi mbalimbali alivyojipatia umaarufu ikiwemo Mambo Mambo na RFA, Je Huu ni uungwana? pamoja na Asili ya Mtanzania kupitia Star TV.

Umahiri wa Baragaza kwenye kupika na kuwasilisha maudhui ulivutia walaji wengi wa habari.

Taarifa zaidi kuhusu msiba huu tutaendelea kukujuza.

R.I.P Juma Baragaza

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments