MARA INVESTORS WAKABIDHI JENGO LA OFISI YA SERIKA YA MTAA KWA JOSHUA NASSARI


Kundi la wadau wa maendeleo Mkoa wa Mara wanaoishi na kufanya kazi sehemu mbali mbali hapa nchini (Mara Investors) limekabidhi jengo kwa ajili ya ofisi ya Serikali ya Mtaa ili kusaidia huduma za kiutawala kwa wakazi wa mtaa wa Serengeti Kata ya Nyatwali Bunda mjini.
Jengo hilo lenye thamani ya Shilingi 15.5 limejengwa kwa msaada wa wadau wa maendeleo wa mkoa Mara ikiwa ni Pamoja ,Dkt. Amon Manyama, Dkt. Sebastian Ndege na Wakili Deus Mgengeli.

Wadau hao wamejitolea kujenga ofisi hiyo ili kusaidia upatikanaji wa huduma za Kiserikali katika ngazi ya mtaa kutokana na mahitaji yanayokuwepo kwa Muda mrefu.Pia linatarajiwa kuwa kituo cha taarifa mbalimbali za kitalii na uwekezaji Katika eneo la Nyatwali,Bunda.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi jengo hilo, Agosti 8,2021 Mkuu wa Wilaya ya Bunda Joshua Nasari aliwashuru wafadhili hao na kuwataka wakazi wa Bunda kupokea kwa mikono miwili ofisi hiyo na kujipanga kwa kumalizia kuongezea kile kilichopungua kwenye ofisi hiyo.

Nasari alisema ofisi hiyo itakuwa ni msaada mkubwa kwa kuwa Pamoja na kutoa huduma za kiserikali kwa wananchi wa eneo hilo, pia itatoa huduma ya taarifa za utalii hususani katika ukanda wa Magrabi mwa Serengeti.
Mkuu huyo wa wilaya aliwashukuru Mara Investors kwa kujitolea kujenga ofisi hiyo na kuwataka wadau wengine kujitokeza katika kusaidia jamii kupambana na changamoto mbali mbali ili kuweza kupata maendeleo.

"Sekta binafsi ni wadau wetu katika maendeleo ya nchi kwa ujumla,Serikali pekee haitoweza kufanikisha.Na nyie wananchi muunge mkono juhudi za serikali kwa kuchapa kazi,kupiga vita uzembe na tabia za umbea na uzururaji'',alisema Nassari.

Pamoja na kushiriki kuzindua ofisi hiyo Nassari hiyo alipata fursa ya kupanda miti kadhaa ikiwa ni ni sehemu ya uhamasishaji wa kutunza mazingira wilayani humo.

Kwa upande wake, Dkt. Amon Manyama, mmoja wafadhili walichangia ujenzi ,alisema yeye Pamoja na wenzake wamejipanga kwa ajili ya kusaidia kufikisha huduma ya maji na Umeme pamoja na miundombinu ya taa za kutumia umeme wa jua (solar) ili kuimarisha na kusaidia shughuli za kiuchumi na kijamii katika eneo la Ndabaka Centre.


Naye mwekezaji kutoka Jembe Group Dkt. Sebastian Ndege aliiomba serikali kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya kusaidia uwekezaji wenye tija unaofanywa na sekta binafsi.Aidha Dr Ndege aliahidi kuendelea kusaidia jitihada mbali mbali za kimaendeleo katika mtaa wa Serengeti kwa kufadhili Ujenzi gati ya Maji safi na Salama na Choo cha Kisasa kwa ajili ya wageni na watalii wanaopita eneo hilo.Aidha amewataka uongozi wa Wilaya kunadili matumizi ya Soko lililojengwa hapo na kuwa gofu,litumike kama soko la kitalii ambapo litatoa ajira kwa vujana na kina mama wa Mtaa huo.

Mwekezaji mwingine kutoka Mara Investors Wakili Deogratius Mgengeli aliiomba serikali kushughulikia kero ya umiliki wa ardhi kupitia Hati za kimila ili ziweze kutumika kupata mikopo ya uwekezaji katika eneo hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments