NANHRI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI , TAASISI KULINDA HAKI ZA RAIA | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, August 4, 2021

NANHRI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI , TAASISI KULINDA HAKI ZA RAIA

  Malunde       Wednesday, August 4, 2021

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Mohamedh Hamad

Na Magrethy Katengu - Dar es salaam
Mtandao wa Taasisi za Haki za Binadamu wa nchi za Afrika (NANHRI) umesema utahakikisha wanashirikiana na serikali na taasisi za kibinadamu ili haki za raia zinakuwa mtambuka ili kuchochea maendeleo ya uchumi wa nchi zote.

Akizungumza Dar es salaam mkurugenzi mwendeshaji wa mtandao wa haki za binadamu barani Afrika Gilbert Sebihogo wakati wa ufunguzi wa semina ya wadau kutoka taasisi za kiserikali na binafsi ambapo amesema semina imeandaliwa kwa lengo kuwajengea uwezo wa namna ya kusaidia raia kufahamu haki zao na kuzilinda.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Mohamedh Hamad amesema suala la haki za binadamu ni la watu wote na serikali ina jukumu kubwa na ni lazima ishirikishe wadau mbalimbali ili haki na ulinzi wa raia ilindwe.


"Pamoja na serikali imekuwa ikihakikisha katika masuala yote yanayohusu sheria au katika wanashirikiana na Mtandao wa watetezi wa haki za kibinadamu na asasi za kiraia kutoa maoni yao kabla sheria au sera haijapitishwa na kusainiwa na Rais", alisema Mohamed.

Kwa upande Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadmu (THRDC) amesema kuna masuala ya kisheria yanahitaji wadau kutoka serikalini kwakuwa ndiyo wanaotunga sheria na mipango ya kitaifa hivyo ni muhimu wawe na mashirikiano ya pamoja ma Azaki katika suala la ulinzi wa haki za raia.

Aidha amesema kila taasisi na Watendaji wake wakifuata misingi ya sheria,kanuni na Utawala Bora misingi ya haki za Binadamu haitaweza kuvunjwa.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post