WIKI YA AZAKI KUANZA OKTOBA 23 DODOMA


Mkurugenzi mtendaji wa  Hakirasilimali , Rachel Chagonja
Wiki ya AZAKI kuanza Oktoba 23 Dodoma.

Na Dotto Kwilasa - Dodoma.

WIKI ya Asasi za kiraia (AZAKI)inatarajiwa  kufanyika Oktoba 23 hadi 29  mwaka huu katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kwa lengo la kuimarisha na kujenga mahusiano mazuri baina ya  serikali,watu binafsi pamoja na Asasi za kiraia katika ujenzi wa taifa.

Hayo yamebainishwa  na Mkurugenzi  Mtendaji wa foundation for civil society (FCS) Francis Kiwanga,wakati akiongea na Jamii kupitia vyombo vya habari huku akifafanua  kuwa lengo la wiki hiyo ni Kubadili mtazamo Kwa wananchi  na kutambua umuhimu wa Asasi za kiraia.

Amesema,katika kufanikisha hilo,jumla ya Azaki 1500 zinatarajia kukutana katika wiki hiyo  kwa kuhusisha mijadala na midahalo mbalimbali  pamoja na maonyesho ya kazi  zinazofanywa na Asasi hizo ikiwa ni Pamoja na masuala ya Msada wa masuala ya kisheria,haki za binadamu na afya. 

"Wiki ya Azaki inatarajiwa kuanza kufanyika Oktoba 23 hadi 29  mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma,tunategemea Asasi za kiraia kutumia fursa hii kutengeneza malengo yao mahsusi kwa manufaa ya jamii ya watanzania,"amesema 

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa  Hakirasilimali , Rachel Chagonja amesema tayari  mipango ya  maandalizi ya wiki ya AZAKI imekamilika huku akieleza kuwa wiki hiyo Pamoja na mambo mengine itahamasisha ukuaji wa uchumi wa nchi.

Akíongea kwa niba ya kamati ya maandalizi ya AZAKI,Mkurugenzi huyo Mtendaji wa Hakirasilimali ametumia nafasi hiyo kuhamasisha jamii kushiriki moja kwa moja Katika maonyesho ya wiki hiyo ili kujifunza masuala mbalimbali.

"Tuna jumla ya Asasi 1500 ambazo tayari zimedhibitisha kushiriki Wiki ya Asasi za kiraia,Kupitia Asasi hizo masuala mengi yanafanyika ambayo pengine jamii haiyajui,nitoe rai kwa jamii kuchangamkia fursa hiyo kujifunza,"anasisitiza.

Naye  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la CBM International Nesia Mahenge ,ameongeza kuwa ili kuleta tija,katika wiki hiyo  kutakuwa na utoaji wa tuzo Kwa mashirika na taasisi ambazo zimekuwa na mchango mkubwa Kwa serikali na tuzo Kwa vyombo vya habari ambavyo  vimekuwa vikitoa taarifa  kuhusiana na kazi za Asasi za kiraia.

"Serikali kupitia FCS imetimiza  jukumu lake kuweka mazingira wezeshi Kwa Asasi za kirai Kwa kufanya kazi Kwa kuzingatia  Sheria na kanuni zilizo wekwa,hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuwezesha jamii kushiriki moja kwa moja Katika masuala ya Maendeleo,"amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments