WAZIRI AWESO –WAKANDARASI WANAOSUASUA KWENYE UTEKELEZAJI WA MIRADI TUTAENDELEA KUWACHUKULIA HATUA | MALUNDE 1 BLOG

Friday, July 2, 2021

WAZIRI AWESO –WAKANDARASI WANAOSUASUA KWENYE UTEKELEZAJI WA MIRADI TUTAENDELEA KUWACHUKULIA HATUA

  TANGA RAHA BLOG       Friday, July 2, 2021
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso akizungumza wakati wa kikao hicho kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mngandilwa

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso akizungumza wakati wa kikao hicho kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa

MKUU wa wilaya ya  Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati wa kikao hicho
Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo akizungumza jambo ewakati wa kikao hicho
Baadhi ya washiriki wakifiatikia kikao kazi cha watumishi wa sekta ya maji mkoani Tanga
Baadhi ya washiriki wakifiatikia kikao kazi cha watumishi wa sekta ya maji mkoani Tanga

 

NA OSCAR ASSENGA, TANGA

Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema kuwa hatashindwa kuendelea kuwachukulia hatua za kinidhamu ikiwemo kuwapokonya kazi wakandarasi wanaosuasua ikiwemo wanaokwamaisha utekelezaji wa miradi ya maji nchini

Kauli hiyo alilitoa wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha watumishi wa sekta ya maji mkoani Tanga ambapo alisema kuwa katika kutekeleza tayari ameshawafuta kazi jumla ya wakandarasi 118 pamoja na makampuni 69 yaliyokuwa yanaendesha miradi ya maji katika maeneo mbalimbali nchini.

Alisema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha inampatia mwananchi huduma ya maji safi na salama karibu na maeneo yake bila ya kulazimika kutembea umbali mrefu lakini uwepo wa huduma ya uhakika.

"Uhandisi wa maji ni pamoja na kufuatilia miradi uliyopewa n a kujiridhisha kama huduma ipo, pale unapo sema Mradi umekamilika basi inamana unatoa maji kwa asilimia 100% na sio ujanja ujanja"Alisema Waziri Aweso.

Aliwataka wataalamu wabadili fikra zao juu ya utekelezaji wa miradi ya maji akitolea mfano miradi ya maji vijijini una sehemu tatu ya kwanza ni chanzo eneo la pili tanki la maji la tatu ni kituo cha usambazaji au kama kuna eneo lenye maji ya mserereko lazima kuwea na eneo la kitibu maji.

“Sasa unajenga chanzo, unajenga tenki la maji, unatandaza vituo vya maji halafu unaangiza pump miezi sita watu wanaona vituo vya maji lakini maji hayatoki unatengeneza malalamiko, manung’uniko na masononeko yalisiyo na ulazima “Alisema Waziri Aweso.

Alisema kumbe wakati unapojenga kwanini usiangize na pampu hata kabla maji hayajaingia kwenye tenki watu wayatumie lakini wanaweza kuyatumia wakati wa ujenzi wa tenki.

“Kwa hiyo hizo ndio fikra ambazo lazima zibadilike kwenye wizara ya maji upojenga intake ya maji agiza pampu ili twende sambamba watu waweze kuyatumia maji kuhakikisha dhamira ya Rais wetu Samia Suluhu inatimilika”AlisemaUsikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post