TRENI YENYE KASI ZAIDI DUNIANI YAZINDULIWA




Treni yenye uwezo wa kusafiri kwa kasi ya kilomita 600 kwa saa imezinduliwa katika eneo la Qingdao nchini China. Treni hiyo ya mfumo wa Magliev iliotengenezwa na shirika la reli nchini China ndiyo treni yenye kasi zaidi duniani CRRC kwa sasa.

‘’Magliev ni neno kwa ufupi lenye maana ya Magnetic Levitation’’. Treni hiyo inaonekana kuelea angani kutokana na nguvu za umeme zinazoifanya kuonekana kuwa juu ya barabara ya reli.
Liang Jianying, naibu meneja na muhandisi mkuu wa shirika la CRRC Sifang, aliambia vyombo vya habari nchini humo kwamba mbali na kasi yake , treni hiyo haina kelele na inahitaji uangalizi mdogo ikilinganishwa na treni zengine zenye kasi ya juu. Mfano wa treni kama hiyo ulifichuliwa kwa vyombo vya habari mwaka 2019.

Mwaka huohuo, China ilitangaza mipango yake ya kuanzisha uchukuzi wa saa 3 katika katika miji yake mikuu. Reli yenye kasi ya juu nchini China ni kipaumbele , ikiwa na lengo la kuunganisha miji yake mikuu kwa treni ili kupunguza muda na gharama za usafiri ndani ya taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu duniani.
Kwa sasa , wastani wa kasi ya treni nchini humo ni kilomita 350 kwa saa, huku ndege zikiendeshwa katika kasi ya kati ya kilomita 800 hadi 900 kwa saa. Treni kama hiyo iliozinduliwa Qingdao inaweza kujaza pengo muhimu lililopo katikati. Hatahivyo kuna kitu kimoja muhimu ambacho ni kizuizi katika ufanisi wake ukosefu wa reli za magliev ambazo hazijakamilishwa.

Kwa sasa China ina reli moja pekee ya mfumo wa Magliev inayotumika kibiashara, na inaunganisha uwanja wa ndege wa Pudong huko Shanghai na kituo cha barabarani cha Longyang mjini humo. Safari hiyo ya kilomita 30 huchukua takriban dakika saba na nusu huku treni hiyo ikisafiri kwa kasi ya kilomita 430 kwa saa moja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments