NHC YATAKIWA KUBUNI MIRADI MIPYA MOROGORO


Na Munir Shemweta, MOROGORO
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amelitaka Shirika la Nyumba la Tifa (NHC) mkoa wa Morogoro kubuni miradi mipya ya ujenzi wa katika mkoa huo ili kuliwezesha shirika kuingiza fedha badala ya kutegemea nyumba za zamani.

Dkt Mabula alitoa kauli hiyo jana mkoani Morogoro wakati akizingumza na watumishi wa ofisi ya shirika hilo mkoa wa Morogoro akiwa katika ziara yake ya kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi kero za ardhi katika mkoa huo.

Alisema haileti maana NHC kutegemea nyumba zake zilizojengwa na mkoloni bila ya kuwa na mipango mipya ya ujenzi itakayowezesha shirika hilo kuwa na nyumba nyingine za kisasa zitakazoliwezesha shirika kujiongezea kipato.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, mkoa wa Morogoro bado una uhitaji mkubwa wa nyumba zikiwemo zile za kupangisha hasa kwenye maeneo mapya na kusisitiza kuwa NHC haina budi kuongeza kasi kwa kubuni miradi mipya itakayosaidia shirika kuongeza kipato.

‘’Kumbe ninyi bado mkoa kizamani yaani hamna mradi wa ujenzi wa nyumba mpya na mnategemea zile za zamani? Mnatakiwa kujiongeza kwa kubuni miradi mipya ili muweze kuongeza mapato ya shirika’’ alisema Dkt Mabula.

Naibu Waziri wa Ardhi Dkt Mabula alimtaka Meneja wa NHC Morogoro Constantine Yuda kwenda katika halmashauri za mkoa huo ili kupatiwa maeneo kwa ajili ya ujenzi wa miradi mipya ikiwemo ya nyumba za watumishi kwenye halmashauri za mkoa huo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments