Breaking

Post Top Ad

Wednesday, July 14, 2021

NAIBU WAZIRI KASEKENYA AKAGUA BARABARA NA KUONGEA NA WANANCHI MKOANI KAGERA

 

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya, akizungumza na wakazi wa kata ya Mutukula wilayani Misenyi mkoa wa Kagera, wakati akikagua barabara ya mpya ya Mutukula hadi Minziro, mpakani mwa Tanzania na Uganda.

Wakazi wa kata ya Mutukula wilayani Misenyi mkoa wa Kagera, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya (hayupo pichani), aliposimama kuzungumza nao wakati akikagua barabara ya mpya ya Mutukula hadi Minziro, mpakani mwa Tanzania na Uganda.

Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashid Mohamed, akielezea jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya (wa pili kushoto), wakati Naibu Waziri huyo akikagua barabara ya Omurushaka, Kyerwa hadi Murongo (KM110), iliyotengewa fedha na Serikali kwa ajili ya kuanza kujengwa kilometa 50 kwa kiwango cha lami.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya (wa pili kulia) akimsikiliza mtaalamu wa vipimo vya ugonjwa wa COVID katika mpaka wa Tanzania na Uganda eneo la Murongo, aliposimama wakati akikagua barabara ya Omurushaka, Kyerwa hadi Murongo (KM 110), iliyotengewa fedha na Serikali kwa ajili ya kuanza kujengwa Kilometa 50 kwa kiwango cha lami.

Muonekano wa sehemu ya barabara ya Kyaka hadi Bugene (KM60), mkoani Kagera.

PICHA NA WUU

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages