TIGO MDHAMINI NI RASMI WA MAWASILIANO KATIKA MAONESHO YA 45 YA BIASHARA YA KIMATAIFA (SABA SABA) KWA MIAKA SITA SASA


KAMPUNI ya simu za mkononi ya Tigo, imedhamini rasmi Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba). 

Tigo imeweka rekodi ya kudhamini maonyesho hayo kwa mwaka wa sita ambapo wateja wa Tigo wataendelea kupata ofa maalum katika msimu huu wa maonyesho ya Saba Saba. Katika maonyesho hayo ya 45 ya biashara ya Kimataifa, mwaka huu yataendeshwa chini ya kauli mbiu ya 'Utengenezaji wa ajira na biashara endelevu'.

 Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Tigo, Woinde Shisael, alisema kuwa Tigo imekuwa Mdhamini wa mawasiliano wa maonyesho hayo na kuweka rekodi ya mwaka wa sita mfululizo. 

Alisema mpango huo ni moja ya malengo ya Tigo ikiwemo kusaidia serikali ukiwa moja ya dhamira kukuza biashara na ukuaji wa viwanda vya ndani kwa ustawi wa uchumi wa nchi. 

Alisema Tigo pia imeshirikiana na watengenezaji wa vifaa vitano kutoa matangazo ya kipekee ya mtandao na simu mahiri kwa maelfu ya wateja wake ambao watahudhuria maonyesho ya biashara katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. 

"Tunapoingia msimu mwingine wa kusisimua wa Sabasaba, tumeandaa matoleo ya kuvutia ya mtandao na simu mahiri kwa wateja wetu. Tumeshirikiana na Xiaomi, Infinix, Samsung, TECNO Mobile na Itel kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma nzuri katika maonyesho haya.

 "Tunatarajia wafanyabiashara watatumia huduma zetu za Lipa Kwa Simu. Kwa kuongezea, wateja wa Tigo Pesa watapata habari juu ya App ya Tigo Pesa, huduma ya Kujitunza fedha na ofa zingine za kufurahisha" alisema Woinde.
Kwa upande wa TANTRADE, Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Twilumba Mlelwa, aliipongeza Tigo kwa udhamini huo. Twilumba alisema kuwa TANTRADE ina bahati kuwa na mshirika wa kuaminika katika sekta ya mawasiliano, na kwamba wanatarajia kuendelea kupata huduma nzuri katika kipindi chote cha maonyesho.

 "Kumekuwa na ongezeko kubwa la masoko, mapato na uwekezaji kwa sababu ya kuongezeka kwa matumizi ya mawasiliano ya simu katika," alisema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments