MAKAMU WA RAIS AAGIZA MKURUGENZI NANYUMBU HAMIS DAMBAYA ASIMAMISHWE KAZI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango, leo Julai 24, 2021 amefanya ziara ya kushtukiza katika stendi ya Mabasi ya Mangaka iliopo Wilaya ya Nanyumbu.

Makamu wa Rais amekasirishwa na uongozi wa Wilaya kufanya upotevu mkubwa wa fedha usiolingana na matokeo ya ujenzi wa mradi huo.Ujenzi wa majengo ya stendi hiyo umetumia shilingi bilioni 2.2 kiasi ambacho Makamu wa Rais amesema hakilingani na ujenzi huo.

Makamu wa Rais amemuagiza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Dkt. Festo Dugange kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu Hamis Dambaya ili kupisha uchunguzi kutoka vyombo husika.

Amesema viongozi hawana budi kusimamia fedha za serikali zinazopelekwa katika maeneo yao ili kuwaletea maendeleo wananchi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments