MSANII HOMA HOMA AMEKUJA KULETA HOMA AFRICA MASHARIKI


Msanii wa Afro Beat,Rhumba,Hip hop na R & B Sawyer Misibumba maarufu kwa jina la Homahoma

Msanii wa Afro Beat,Rhumba,Hip hop na R & B Sawyer Misibumba maarufu kwa jina la Homahoma kutoka nchini Congo ambaye makazi yake ni huko nchini Ubelgiji ni mmoja wa msanii wenye talanta ya kipekee sana kuanzia uandishi wake katika muziki.

Homahoma aliamua kufanya mziki rasmi tangu mwaka 2019 ambapo aliachia kazi yake ya “Baby Dose” iliyofanikiwa kwa kiasi flani na baadaye kuja kuachia kazi yake nyingine ambayo ilipewa jina la “Pakadjuma” ambayo ilikuwa na miondoko ya Afro Beat huku akivutiwa na wasanii kama Wizkid pamoja na Burnaboy kutoka Nigeria.

Talanta ya Homahoma ilianza kuonekana baada ya msanii huyu kuwa mpenzi sana wa muziki wa Papa Wemba,Koffi Olomide kutoka Congo  lakini pia katika kizazi chake alipendezwa zaidi na muziki wa Kanyewest,Stromae na Amigos.

Homahoma ameachia kazi yake mpya kutoka kwenye Ep yake iitwayo “Hopium” na wimbo huo unaitwa Uio. karibu utazame na unaweza kufuatilia kazi zake kupitia youtube channel yake pamoja na mitandao ya kijamii kwa jina la @officialhomahoma.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments