WAZIRI UMMY : AJIRA MPYA ZIMEPUNGUZA UHABA WA WALIMU WA SAYANSI | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, July 14, 2021

WAZIRI UMMY : AJIRA MPYA ZIMEPUNGUZA UHABA WA WALIMU WA SAYANSI

  Malunde       Wednesday, July 14, 2021


Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Ummy Mwalimu amesema kwa Sasa hakuna Shule ya Sekondari ambayo haina Mwalimu wa Sayansi.

Waziri Ummy amesema katika ajira 6,749 zilizotewa Mwezi Juni 2021, Walimu wa Fizikia walioajiriwa ni 1,360 na Walimu wa Hisabati Ni 599 ambao wamesambazwa katika shule ambazo hazikuwa na Walimu hao hapo awali.

“Ni imani yangu sasa hakuna shule yoyote ya Sekondari nchini ambayo haina mwalimu wa sayansi hata mmoja,”amesema.

Hata hivyo, ameiaagiza Mikoa kumleta taarifa iwapo kuna Shule ya Sekondari katika Halmashauri ambayo haina Mwalimu wa masomo ya Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati hata mmoja ili ufanyike msawazo wa walimu wa Sayansi.

Aidha, amesema katika mwaka huu wa fedha 2021/22 serikali inatarajia kuajiri walimu 10,000 na kipaumbele kitakuwa walimu wa Sayansi.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post