MAZISHI YA TB JOSHUA KUFANYIKA IJUMAA HII... TUKIO LA KUWASHA MISHUMAA KUPEPERUSHWA LIVE | MALUNDE 1 BLOG

Monday, July 5, 2021

MAZISHI YA TB JOSHUA KUFANYIKA IJUMAA HII... TUKIO LA KUWASHA MISHUMAA KUPEPERUSHWA LIVE

  Malunde       Monday, July 5, 2021
Maelezo ya picha,TB Joshua
Temitope Balogun JoshuaJe maarufu TB Joshua

Tukio la kuwasha mishumaa litaanzisha utararibu wa mazishi ya aliyekuwa muhubiri mashuhuri wa Nigeria, na muasisi wa kanisa la Synagogue Church of All Nations (SCOAN) aliyefariki mwezi uliopita.

Mchungaji TB Joshua alifariki tarehe 5 Juni,2021 akiwa na umri wa miaka 57, siku chache kabla ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

 Mazishi yake yanatarajiwa kuwa ya faragha Ijumaa Julai 9, 2021.

Hata hivyo kanisa lake bado halijafichua ni nini kilichosababisha kifo chake.

Taarifa iliyotolewa na kanisa lake - Synagogue Church of All Nations imesema: "Mungu amemchukua mtumishi wake Nabii TB Joshua nyumbani - sawa na mapenzi yake. Aliutumia muda wake wa mwisho duniani katika huduma ya Mungu. Alifanya alichopaswa kufanya, akakiishi na amekufa kwa ajili yake ."

"Nabii TB Joshua ameacha urithi wa huduma na kujitolea kwa ajili ya ufalme wa Mungu ambao utaendelea kuishi kwa vizazi ambavyo havijazaliwa ."

Mchakato wa kuwasha mishumaa utakuwa utakuwa ni sherehe ya kibinafsi , limesema kanisa la Synagogue Church of All Nations.

Tukio hilo linatarajiwa kuanza saa kumi na mbili unusu jioni Jumatatu kwa saa za Nigeria.

Litapeperushwa pia moja kwa moja kwenye chaneli ya TV ya kanisa hilo.

Kulingana na taarifa hiyo Kanisa hilo limewataka watu kubeba mishumaa kama ishara ya kuungana katika mpango wa ‘’kumheshimu’’ mtumishi wa Mungu - TB Joshua."

Chanzo - BBC Swahili
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post