MOTO WAIBUKA KANISANI KWENYE IBADA YA KUAGA MWILI WA TB JOSHUA


Temitope Balogun JoshuaJe maarufu TB Joshua

Moto umewaka usiku wa Jumatatu katika ghala lililopo ndani ya kanisa la mhubiri aliyekuwa na ushawishi mkubwa nchini Nigeria TB Joshua mjini Lagos.

Moto huo ulitokea wakati wa mchakato wa mazishi yake ulioanza jana kwa kuwashwa mishumaa kwa ajili ya kumuenzi Nabii TB Joshua aliyefariki mwezi uliopita akiwa na umri wa miaka 57.

Moto uliwaka wakati wa ibada ya iliyokuwa sehemu ya mazishi ya TB Joushua iliyoongozwa na mjane wake Everlyne Joshua.

Waombolezaji na waumini waliokusanyika katika kanisa lake la Synagogue Church of All Nations kwa ibada ambayo iliongozwa na mjane wa TB Joshua Evelyn Joshua walikanyagana walipokuwa wakitimua mbio kuokoa maisha yao.

Kanisa hilo limesema moto huo ulitokana na hitilafu ndogo ya umeme. Limesema moto huo umezimwa na hapakuwa na mtu yeyote aliyeathiriwa na moto huo.

TB Joshua atazikwa katika eneo la kanisa hilo Ijumaa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments