ASAKWA NA POLISI KWA KUMBAKA KISHA KUMUUA MTOTO WA MIAKA MITANO | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, July 6, 2021

ASAKWA NA POLISI KWA KUMBAKA KISHA KUMUUA MTOTO WA MIAKA MITANO

  Malunde       Tuesday, July 6, 2021

Mkazi wa kijiji cha Mutuka wilayani Babati Mkoa wa Manyara, Emmanuel Naasi (30) anasakwa na polisi akituhumiwa kumbaka na kumuua mtoto wa kaka yake mwenye umri wa miaka mitano.

Akizungumza leo Jumanne Julai 6, 2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Merrison Mwakyoma amesema tukio hilo limetokea jana Julai 5, 2021 saa 12 jioni na kwamba Naasi alikutana na mtoto huyo na wenzake wawili wakitoka kuchota maji na kuanza kuwakimbiza.

“Kila mmoja alikimbilia upande wake lakini yeye alimkamata marehemu, alimbaka na kisha alimpiga na kitu kizito usoni na mtoto huyo akafariki dunia papo hapo,” amesema kamanda Mwakyoma akibainisha kuwa baada ya kitendo hicho, mtuhumiwa huyo alikimbia.

Via Mwananchi
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post