MWANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE ATUHUMIWA KUMUUA MAMA YAKE MZAZI KISHA KUMNG'OA MACHO KILIMANJARO

Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Kindi wilayani ya Moshi mkoani Kilimanjaro anatuhumiwa kumuua mama yake mzazi Marietha Mushi (62) kwa kumnyonga na shuka, kumpiga na kitu kizito kichwani kisha kumng’oa macho.

Taarifa imeelezwa kuwa mama huyo alikuwa na ulemavu wa mkono jambo linaelezwa kuwa limechangia ashindwe kujitetea wakati akishambuliwa na binti yake huyo.

Akizungumza na chombo kimoja cha habari Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Said Mtanda, amesema tukio hilo limetokea Julai 5, 2021 katika eneo la Kibosho Sambarai.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments