WATU 284 KATI 408 WANAOUGUA CORONA TANZANIA WANATUMIA MITUNGI YA OKSIJENI | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, July 10, 2021

WATU 284 KATI 408 WANAOUGUA CORONA TANZANIA WANATUMIA MITUNGI YA OKSIJENI

  Malunde       Saturday, July 10, 2021

Tanzania imeanza kutoa takwimu ya watu walioambukizwa virusi vya corona ambapo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima amesema hadi kufikia Julai 8, 2021 jumla watu 408 walibainika kuwa na ugonjwa wa Corona huku 284 wakitumia mitungi ya Hewa ya Oksijeni.

Dk Gwajima ametoa taarifa hiyo leo Jumamosi Julai 10, 2021 wakati akitoa elimu ya kujikinga na ugonjwa huo kwenye mnada wa Msalato jijini Dodoma.

Rais Samia Suluhu Hassan mara kwa mara amekuwa akiwakumbusha Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari na kujilinda dhidi ya wimbi la tatu la janga la corona.

Katika moja ya ziara yake akiwa njiani kutoka Dodoma Rais Samia alielezea kushangaa kuona mamia ya watu bila barakoa.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post