BILIONEA BOSI WA KAMPUNI YA AMAZON ARUKA ANGA LA JUU ZAIDI KWA ROKETI YAKE | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, July 20, 2021

BILIONEA BOSI WA KAMPUNI YA AMAZON ARUKA ANGA LA JUU ZAIDI KWA ROKETI YAKE

  Malunde       Tuesday, July 20, 2021

Roketi aina ya Blue Origin, ikiwa na Jeff Bezos na wafanyakazi ndani, ikiwa inapaa kutoka ardhini.

Tajiri mkubwa duniani na Muanzilishi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Amazon Jeff Bezos amefanikiwa kwenda kwenye anga la juu zaidi na kurudi duniani ndani ya dakika 11 kwa kutumia roketi iliyotengenezwa na kampuni yake akivunja rekodi iliyowekwa na Bilionea Richard Branson mapema mwezi huu.

Bezos na pamoja na watu wengine watatu, walipaa na chombo maalum kisicho kuwa na rubani kwenda kwenye anga la juu zaidi duniani.

Mnamo tarehe 11 Julai, 2021 Billionea Sir Richard Branson alifanikiwa kufikia ukingo wa anga za juu kutumia roketi ya Virgin Galactic na kuweka rekodi ambayo imevunjwa leo na tajiri mwenzake Jeff Bezos.
Tajiri Jeff Bezos na wenzake watatu wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kupaa angani
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post