Breaking

Post Top Ad

Saturday, June 12, 2021

SEKTA YA UJENZI YASHIRIKI BONANZA LA PAMOJA LILILOANDALIWA NA BENKI YA CRDB

 

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya (wa nne kulia), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na watumishi wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi) katika bonanza la pamoja la Watumishi wa Serikali, Waheshimiwa Wabunge, Wafanyakazi wa Benki ya CRDB na wananchi,lililofanyika leo Juni 12,2021 jijini Dodoma.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Tulia Ackson (wa nne kulia), katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), katika bonanza la pamoja lililoandaliwa na Benki ya CRDB,lililofanyika Juni 12,2021 Jijini Dodoma.

Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) wakifurahia ushindi wa watumishi wa Sekta hiyo (hawapo pichani), mara baada ya kushinda shindano la kukimbia na gunia katika Bonanza la Pamoja lililoandaliwa na Benki ya CRDB,lililofanyika leo Juni 12,2021 Jijini Dodoma.

Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), wakiwa katika picha ya pamoja katika Bonanza lililoandaliwa na Benki ya CRDB,lililofanyika leo Juni 12,2021 Jijini Dodoma.

Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi( Sekta ya Ujenzi) wakishiriki mashindano ya kukimbia na magunia ambapo kwa Sekta ya Ujenzi ilishika nafasi ya pili katika Bonanza la Pamoja lililoandaliwa na Benki ya CRDB,lililofanyika leo Juni 12,2021 jijini Dodoma.

PICHA NA WUU

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages