SIMBACHAWENE ARIDHISHWA NA KASI UJENZI MAKAZI YA ASKARI ZIMAMOTO, KUKAMILIKA SEPTEMBA 2021


 Na Mwandishi Wetu, MoHA, Dodoma
KATIKA kukabiliana na uhaba wa nyumba za watumishi nchini, Serikali imetoa shilingi bilioni tano kwa ajili ya ujenzi wa makazi  ya Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika eneo la Kikombo Jijini Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amezungumza hayo, jijini Dodoma, leo, mara baada ya kukagua ujenzi huo huku akifurahishwa na kuridhishwa namna ambavyo ujenzi unavyoendelea.

Alisema ameridhika na namna ya gharama za ujenzi wa makazi hayo yenye majengo sita na gharama zinavyokwenda na kujidhihirisha kwamba bilioni tano zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan zinatumika kiuhalali na fedha hizo zitamaliza ujenzi huo.

“Nimefurahishwa sana na kasi ya ujenzi, nimeridhika na ujenzi unaoendelea ujenzi wa mradi huu wa nyumba za Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, nikupongeze Kamishna Jenerali kwa kusimamia vema fedha za Serikali inaonyesha dhahiri kwamba kazi itakamilika kwa ufanisi,” alisema Simbachawene.

Kwa upande wake, Kamishna Jenerali, John Masunga alisema nyumba hizo zinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi wa tisa mwaka na askari pekee ndio watakaa katika makazi hayo na sio maafisa.

Alisema kukamilika kwa nyumba hizo itakuwa mkombozi mkubwa kumaliza kilio cha wa Askari ambao wanakabiliwa na makazi ya kuishi na kwamba nyumba hizo ni maalumu kwa Askari wa chini na ambao wanafanya kazi ofisi ya Makao Makuu na kituo cha Zimamoto na Uokoaji kilichopo Chamwino.

“Tunaishukuru sana Serikali kupitia Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutatua changamoto hii na kutupatia fedha hizo tunamuahidi  tutajitahidi tunamaliza makazi haya kwa wakati,” alisema CGF Masunga.

Akisoma taarifa ya miradi inayotekelezwa na Jeshi hilo, Mmliki Majengo wa Jeshi hilo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Julius Ntabala alisema kuwa Jeshi hilo kwa Mwaka 2020/21 linatekeleza miradi mitatu ikiwemo Kituo cha Zimamoto na Uokoaji eneo la Chamwino, ujenzi wa Kituo cha Zimamoto na Uokoaji eneo la Nzuguni na mradi wa Makazi ya Askari Kikombo.

Akifafanua namna mradi ulipofikia alisema ujenzi makazi ya Kikombo yako hatua ya asilimia 55 ambayo ipo hatua ya kupaua na kuanza kazi za ndani na nje na kwamba kwa sasa kazi inayoendelea ni ufungaji wa nondo za sakafu ya ghorofa ya nne na kisha kumwaga zege la nguzo na kupandisha kuta na kuweka mkanda wa mwisho.

“Ujenzi unaendelea vizuri gharama zilizotumika mpaka sasa ni shilingi 4,006,486,300.00 mbali na jitihada hizi tumekumbana na changamoto ya kupanga kwa gharama za saruji ambapo kumeathiri mradi na tutakapofika mwishoni tutaona mapungufu ni kiasi gani kimepungua ili tuombe fedha ya nyongeza,” alisema Ntabala.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments