SERIKALI YAWAAGIZA MAMENEJA WA FEDHA WA MAMLAKA ZA MAJI KUIMARISHA MIFUMO YA USIMAMIZI WA FEDHA | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, June 17, 2021

SERIKALI YAWAAGIZA MAMENEJA WA FEDHA WA MAMLAKA ZA MAJI KUIMARISHA MIFUMO YA USIMAMIZI WA FEDHA

  Malunde       Thursday, June 17, 2021

Serikali imewaagiza mameneja wa fedha kutoka katika Mamlaka za Maji nchini kuimarisha mifumo ya usimamizi wa fedha hususani za utekelezaji wa miradi ya sekta hiyo ili kudhibiti matumizi mabaya na miradi kuwa yenye tija.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa raslimali watu kutoka Wizara ya Maji, Barnabas Nduguru wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha mameneja fedha kutoka Mamlaka zote za maji hapa nchini kilichofanyika mkoani Tanga.

Amesema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha wanatatua kero ya uhaba wa maji safi na salama hivyo Mameneja fedha ndiyo kiungo muhimu katika kuhakikisha dira na sera ya maji inaweza kufikiwa kwa vitendo.

Amesema kuwa kwa kutumia mabadiliko ya Udhibiti na Usimamizi wa rasilimali fedha yanayoendelea kwa sasa katika sekta mbalimbali nchini hivyo ni jukumu lao kuimarisha usimamizi wa mapato na fedha za serikali kwa lengo la kumaliza kero ya maji kwa wananchi.

Pia amewataka kuwa na ushirikiano katika majukumu yao ili kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.

Amesema kuwa mameneja hao ndiyo chachu ya usimamizi, ushauri na utekelezaji wa miradi ya maji kwenye mamlaka zake hivyo wana wajibu wa kutokuwa vikwazo kwa kuchelewesha utoaji wa fedha kwa wakati za miradi na hivyo kusababisha kutokamilika kwa wakati.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post