RC MAKALLA AWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, June 24, 2021

RC MAKALLA AWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA

  Malunde       Thursday, June 24, 2021


 Kufuatia kuwepo kwa Viashiria vya Mlipuko wa Ugonjwa wa Corona, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewataka Wananchi kuchukuwa tahadhari na kuziagiza Taasisi na sehemu zote za mikusanyiko kuweka ndoo za Maji na Miundombinu ya Maji tiririka.


Akitoa tamko la tahadhari dhiri ya Corona RC Makalla amesema Kutokana na Mwingiliano wa watu kutoka Nchi jirani na Nchi mbalimbali na Mikoa mingine wameona ni vyema kutoa tahadhari kwa Wananchi.


Miongoni mwa tahadhari ambazo RC Makalla amewataka Wananchi kuzichukuwa ni pamoja na :-


1.Kuvaa kwa Usahihi Barakoa kila wawapo sehemu za mikusanyiko, vyombo vya usafiri, Masoko, sherehe, maofisini na vituo vya Afya.


2. Kunawa Mikono kwa Maji tiririka kwa sabuni Mara kwa Mara.


3.Wananchi kuwahi mapema vituo vya Afya wanapobaini dalili za Corona ikiwemo homa Kali, mafua Makali, kikohozi, uchovu na nyingine.


4. Kufanya Mazoezi ili kuimarisha Kinga ya Mwili.
5. Kula mlo kamili.
6. Uangalizi mzuri kwa watu walio kwenye hatari ya kupata madhara* wakiwemo Wazee na Wenye Magonjwa sugu.


Aidha RC Makalla amewaelekeza Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Taasisi za Umma na za kiraia na Vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanasimamia ipasavyo maelekezo hayo.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post