RAIS SAMIA AWASIMAMISHA KAZI VIONGOZI SOKO LA KARIAKOO - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Tuesday, June 1, 2021

RAIS SAMIA AWASIMAMISHA KAZI VIONGOZI SOKO LA KARIAKOO


Rais Samia Suluhu Hassan ameusimamisha kwa muda  uongozi wa soko la Kariakoo lililopo jijini Dar es salaam, na kuagiza uchunguzi ufanyike kuhusu tuhuma mbalimbali zinazoukabili uongozi huo.

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza hatua hiyo wakati wa ziara yake ya kushtukiza katika soko hilo, ambapo pia amesikiliza kero za Wafanyabiashara mbalimbali wa soko hilo.

Amesema hali ya soko hilo la Kariakoo hairidhishi, na kwamba Serikali kwa sasa inaenda kufanya tahmini ya kina kuona namna ya kuliendesha soko hilo.

Rais Samia Suluhu Hassan amesema lengo la kuanzishwa kwa soko hilo ni kuwasadia Wafanyabiashara wadogo, lakini kwa sasa jambo hilo halipo na kinachofanyika ni kuwanufaisha viongozi wa soko hilo pekee.

Ameongeza kuwa mpangilio wa bidhaa ndani ya soko hilo ni mbaya, jambo ambalo linahitaji kufanyiwa marekebisho ya haraka.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages