Breaking

Post Top Ad

Sunday, June 20, 2021

RAIS SAMIA ATEUA WAANDISHI WA HABARI KUWA WAKUU WA WILAYA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Jumamosi Juni 19,2021 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilayanchini ambapo amewabadilisha vituo vya kazi baadhi, ameingiza sura mpya na kuwarudisha waliowahi kushika nafasi hizo.

Katika orodha hiyo, Rais Samia amewateua waandishi wa habari kushika nafasi hiyo. Walioteuliwa ni Fatma Almas Nyangasa wa Azam TV (Kigamboni), Simon Simalenga wa Clouds Media Group (Songwe) na Abdallah Mwaipaya wa ITV/Radio One (Mwanga).


Gabriel Zakaria Olemegili kutoka TBC kuwa Mkuu wa Wilaya ya Busega na Mohamed Ngoma kutoka Clouds Media amemteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi, kabla ya uteuzi huo Ngoma alikuwa DAS Singida.

Wakuu wa Wilaya wateule wataapishwa kuanzia tarehe 21 Juni, 2021 saa nne (4) asubuhi na Wakuu wa Mikoa yao.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages