MKURUGENZI MKUU TBS : WATANZANIA MSINUNUE BIDHAA BILA KUHAKIKI ALAMA YA UBORA

 

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS)  Dkt Yusuph Ngenya akizungumza na waandishi wa habari

NA OSCAR ASSENGA, TANGA

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS)  Dkt Yusuph Ngenya ametoa wito kwa  watanzania wasinunue bidhaa yoyote bila kuhakikisha kwamba ina alama ya ubora kwa bidhaa zinazozalishwa nchini.

Ngenya aliyasema hayo eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea maonyesho ya nane ya Biashara ambapo alisema hatua hiyo itasaidia kuwaondolea hasara ambazo wamekuwa wakikumbana nazo kutokana na bidhaa wanazonunua kutokuwa na ubora unaotakiwa.

Alisema kwani bidhaa zimekuwa na athari nyingi katika matumizi ya binadamu hiyo ni muhimu watanzania kutambua kwamba wanaponunua bidhaa wanapaswa kuzikagua na kuona kama zina ubora unaotakiwa ili kuweza kuepukana na majanga ambayo yanaweza kuwakuta kutokana na bidhaa  feki.

“Lakini hata katika operesheni zetu ambazo tumekuwa tukizifanya tunagundua  bidhaa gani ambazo zinaingizwa kwenye masoko na hazina ubora ikiwemo bidhaa za ujenzi ,vifaa vya umeme vingi vinakuja feki hivyo tujitahidi kuvitambua na kuviondoa kwenye soko kwani mfano vifaa vya umeme madhara yake vinaweza kushika moto na kuweza kuharibu mali”Alisema Mkurugenzi huyo wa TBS

Akizungumzia lengo la uwepo wao kwenye maonyesho hayo ya nane ya biashara alisema wapo kwa ajili ya kuwaelimisha wananchi kuhusu shughuli za TBS na namna ya kupata huduma zao

“TBS pamoja na mambo megine kwenye maonyesho kama haya tunawakaribisha wananchi kuweza kuwaelimisha kwa mfano wale wanaotaka kupata huduma za TBS ikiwemo  bidhaa zao ziweze kupata alama ya ubora lakini pia tunashughulikia uuzaji wa bidhaa za chakula na vipodozi kuweza kupata usajili wa shughuli zao”Alisema Mkurugenzi huyo mkuu wa TBS.

Hata hivyo aliwataka wajasiriamali watengenezaji  wa bidhaa ndogo ndogo ni rahisi kwanza kwenda sido kupata mafunzo ambayo yatawasaidia kupata cheti  kitachowawezesha kupata barua kutoka sido na baadae waende   TBS kuweza kutambulika na wao watafanya kazi iliyobakia mpaka kuhakikisha bidhaa yao inapata ubora.

Mwisho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments