FAMILIA YAFUKUA MWILI WA NDUGU YAO ALIYEZIKWA KWA SIRI NA MCHEPUKO

Mwili wa mwanaume mwenye umri wa miaka 71 umefukuliwa katika kaunti ya Nyeri nchini Kenya baada ya kubainika kuwa alizikwa na mwanamke ambaye ni mpango wake wa kando 'mchepuko'.

Inaelezwa kwamba marehemu Hudson Wanjohi Ndumia aliaga dunia mnamo Mei 10 na kuzikwa Mei 22,2021 na mpenzi wake wa kando ambaye alikuwa akiishi naye Kagongo, Eneobunge la Tetu katika kaunti ya Nyeri. 

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 50 anatuhumiwa kuwasilisha stakabadhi ya mazishi akiuchukua mwili wa Ndumia katika makafani Mathari Consolata Mission huko Nyeri, pasi na kuwajulisha familia. 

Hii ni baada ya familia yake kubaini kwamba mpendwa wao alikuwa amezikwa bila wao kujua.

 Duru za kuaminika zilisema kwamba, Ndumia, anayetoka Makuyu katika kaunti ya Murang’a, aliishi na mpenzi wake wa siri, mjane, huko Tetu, kaunti ya Nyeri.

Ndumia alidaiwa kuzozanana mkewe na ndiposa akaamua kuhama.

 Familia ya marehemu ilipata kibali cha kufukua maiti kutoka mahakamani wiki iliyopita baada ya kugundua kwamba mpendwa wao aliaga dunia na kuzikwa tayari. 

Mahakama ya Nyeri ilikubailiana na ombi lao na kuwapa kibali Ijumaa, Juni 18.

 Nduguye marehemu, Samuel Ndumia, aliwaambia waandishi wa habari kwamba hatimaye wana furaha kwani watampa mpendwa wao mazishi ya kiheshima. 

Maafisa wa polisi wa kupambana na ghasia walisimamia shughuli ya kufukua mwili huokwenye shughuli iliyofanyika Ijumaa, Juni 25.

Familia ya Ndumia ilisema wanashuku huenda mwenda zake alipoteza aisha yake kutokana na majeraha aliyoyapata wakitandikana na mpango wake wa kando. 

"Kabla ya kifo chake, ndugu yetu alikuwa amelazwa hospitalini na majeraha ya moto kwenye sehemu zake za siri. Tunashuku alipata majeraha wakati wa makabiliano na mwanamke ambaye alikuwa akiishi naye,” alisema Samuel Ndumia. 

Familia hiyo ilisema kuwa ilikuwa inasubiri matokeo ya upasuaji wa maiti yake Ndumia walipogundua alizikwa kisiri.

CHANZO - TUKO NEWS

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments