WANANDOA WAFARIKI DUNIA BAFUNI



Wanandoa hao wapya Zaheer Sarang na Nabeelah Khan (24) wamefariki dunia kwa shoti ya umeme huko Afrika kusini ikiwa ni siku moja tu tangu watoke kula fungate ‘honeymoon’.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa polisi wa jimbo la Guetang, Mavela Masondo alisema miili ya wanandoa hao iligunduliwa bafuni kwao Jumapili Juni 13, mwaka huu.

Ilisema wanandoa hao wakiwa bafuni mke huyo alishika tap/switch akapigwa na shoti ya umeme ambapo mume alipojitosa kumuokoa na yeye akaunganishwa katika shoti hiyo wakafariki wote.

Aidha, taarifa za awali zinaeleza kuwa maeneo hayo watu hupenda kujiunganishia umeme kiholela kinyume na sheria na hivyo kusababisha majanga kama hayo.

Hata hivyo, polisi wamesema bado wanaendelea kuchunguza zaidi tukio hilo kwa kushirikiana na mamlaka inayohusika kusambaza umeme katika jimbo la Guetang.

STORI NA MUSHI GABRIEL | GPL

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments