TAZAMA HAPA MAJINA 9,675 YA WALIMU WAPYA & WATUMISHI WA AFYA WALIOPANGIWA VITUO VYA KAZI 2021

 

Serikali ya Tanzania imetangaza watumishi wapya 9,675 wa kada za elimu na afya walioajiriwa kufuatia kibali cha ajira kilichotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan, Aprili, 2021.

Majina ya walimu waliopangiwa vituo vya kazi yanapatikana katika tovuti ya ofisi ya Rais-Tamisemi ya www.tamisemi.go.tz

Watumishi hao wapya wametangazwa na katibu mkuu ofisi ya rais Tamisemi, Profesa Riziki Shemdoe.

Profesa Shemdoe ametangaza ajira za elimu 6,749 kwa shule za msingi na sekondari na wataalamu wa afya 2,726.

Amesema waombaji wa kada ya ualimu walikuwa 99,583 na wataalam 37,437 wa kada ya afya wakiwemo wenye ulemavu 1,099 waliomba nafasi hizo.

“Baada ya kukamilisha taratibu zote za uchakataji wa maombi walimu 6,949 (3,949 wa shule za msingi na 3,000 wa shule za sekondari) na wataalam wa kada za afya 2,726 wamepangiwa vituo vya kazi,” amesema Profesa Shemdoe

Kuona Orodha ya Walimu  Bofya hapa   posted-applicants - 2021-06-25.pdf

Kuona Orodha ya Kada ya Afya Bofya hapa   ORODHA YA WATUMISHI WA AJIRA MPYA KADA YA AFYA 25 JUNI, 2021.pdf


Tazama Majina yote <<Hapa<<

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments