Picha : TGNP YAENDESHA MJADALA 'KIJIWE CHA KAHAWA' BAJETI YA TAIFA 2021/2022 IKIWASILISHWA MUBASHARA BUNGENI

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akifungua Mjadala wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022 (Kijiwe cha Kahawa), uliofanyika leo Alhamis Juni 10,2021 katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umeendesha Kijiwe cha Kahawa kwa ajili ya kuwapa fursa wadau mbalimbali wa haki za wanawake na masuala ya jinsia kufuatilia Hotuba ya Bajeti ya Taifa mwaka wa fedha 2021/2022 Mubashara ikiwasilishwa Bungeni na kutoa maoni, mitazamo yao juu ya bajeti na mapendekezo yao yatakayowezesha uboreshaji wa utekelezaji wake kwa mrengo wa kijinsia.

Mjadala huo ulioongozwa na Kauli Mbiu "Bajeti yenye Mrengo wa Kijinsia : Chachu ya uchumi Jumuishi, Viwanda na Maendeleo ya watu" umekutanisha pamoja na mashirika yanayohusika na kutetea haki za wanawake, wanachama wa Vituo vya Taarifa na Maarifa,Wanachama wa Semina za Jinsia na Maendeleo, Wanazuoni, Serikali za mitaa, Madiwani, Wana Jamii, Wawakilishi wa sekta binafsi,vyombo vya habari, Wafanyakazi na Wanachama wa TGNP na Wadau wa Maendeleo.

Akifungua Mjadala wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022, uliofanyika leo katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi amesema mjadala huo unalenga kutathamini Bajeti ya Taifa mwaka 2020/2021 kwa mtizamo wa kijinsia na kwa kuzingatia matarajio ya wananchi na kubainisha mapengo ya kijinsia yaliyopo katika bajeti na kutoa mapendekezo ya namna ya kuendelea kufuatilia mchakati wa utekelezaji wa bajeti ya matokeo yake.

“Jukwaa hili la Kijiwe cha Kahawa limewaleta pamoja wadau mbalimbali kutazama na kusikiliza Mubashara uwasilishwaji wa taarifa ya hali ya uchumi mwaka 2020 kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Hotuba ya Bajeti ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022”,amesema Lilian.

“Mjadala huu umelenga kuhamasisha nguvu na sauti za pamoja katika kudai utengwaji wa rasilimali ulio jumuishi ili kutatua changamoto za makundi mbalimbali katika jamii hasa ya walio pembezoni”,amefafanua Lilian.

Amesema Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa miaka mitano sasa umekuwa ukiandaa Jukwaa hilo ambalo ni mojawapo ya majukwaa ya TGNP ya kujenga nguvu za pamoja ili kuleta chachu ya mabadiliko chanya kisera, kiutendaji na kifikra kwa mrengo wa jinsia.

Katika hatua nyingine amesema kwa miaka 27 sasa TGNP imekuwa mstari wa mbele katika kujenga uwezo na ushawishi juu ya bajeti yenye mrengo wa kijinsia ambapo TGNP imekuwa ikijihusisha na mchakati wa bajeti kila mwaka kwa kuwawezesha wanawake na makundi yaliyo pembezoni katika ngazi za jamii kushiriki kikamilifu kupitia mchakato wa fursa na vikwazo unaofanyika katika ngazi ya jamii.

“Mchakato huu unawezesha wananchi kuibua vipaumbele vyao na pia kuwaunganisha na mjadala wa kitaifa ili kudai utengwaji wa rasilimali kwa ajili ya masuala ya jamii kwa ujumla. Kwa kushirikiana na wadau tumewezesha kwa pamoja uingizwaji wa masuala ya jinsia katika bajeti za baadhi ya halmashauri, Wizara na bajeti ya taifa”,ameongeza

Amesema Jukwaa hilo litaimarisha sauti za pamoja katika kuhamasisha bajeti yenye mrengo wa kijinsia kwa maendeleo endelevu.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi huyo wa TGNP ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuyapa kipaumbele masuala ya Kijinsia.

“Masuala ya kijinsia yamekuwa kipaumbele katika uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. Ni jukumu letu sote kuhakikisha tunafuatilia, inapofika mwaka 2025 tuone kuna mabadiliko kwa wanawake. Tuchukue fursa hii ya serikali ya awamu ya sita kuhakikisha tunakuwa mfano katika usawa wa kijinsia na watu wengine kutoka nchi zingine duniani zije kujifunza Tanzania”,amesema Lilian.

Naye Mwanachama wa TGNP Jovita Mlay amewataka wadau wa haki za wanawake na masuala ya jinsia kuendele kupaza sauti kwenye maeneo yenye changamoto ili serikali iweze kuzitafutia ufumbuzi  akibainisha kuwa Rais Samia ameonesha wazi kuwa anazingatia masuala ya usawa wa kijinsia.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akifungua Mjadala wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022 (Kijiwe cha Kahawa), uliofanyika leo Alhamis Juni 10,2021 katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akifungua Mjadala wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022 (Kijiwe cha Kahawa), uliofanyika leo Alhamis Juni 10,2021 katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.
Wadau wa haki za wanawake na masuala ya kijinsia wakiwa ukumbini wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022 (Kijiwe cha Kahawa), uliofanyika leo Alhamis Juni 10,2021 katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.
Mchambuzi wa Masuala ya Kijinsia, Edward Mhina akiwasilisha masuala muhimu ya kijinsia kuhusu hali halisi ya uchumi wa taifa wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022 (Kijiwe cha Kahawa), uliofanyika leo Alhamis Juni 10,2021 katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.

Wadau wa haki za wanawake na jinsia wakifuatilia uwasilishwaji Mubashara wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022 Bungeni Dodoma  kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba wakiwa katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.

Mwanachama wa TGNP, Jovita Mlay akichangia hoja wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022  uliofanyika leo Alhamis Juni 10,2021 katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.

Mwanachama wa TGNP, Maimuna Kanyamala akichangia hoja wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022  uliofanyika leo Alhamis Juni 10,2021 katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Programu TGNP, Shakila Mayumana akichangia hoja wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022  uliofanyika leo Alhamis Juni 10,2021 katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.
Wadau wa haki za wanawake na jinsia wakifuatilia uwasilishwaji Mubashara wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022 Bungeni Dodoma  kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba wakiwa katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.
Wadau wa haki za wanawake na masuala ya kijinsia wakiwa ukumbini wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022 (Kijiwe cha Kahawa), uliofanyika leo Alhamis Juni 10,2021 katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.
Mkurugezi wa shirika la Afya Plus, Suzan Yumbe akichangia hoja wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022  uliofanyika leo Alhamis Juni 10,2021 katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.
Mdau Rose Kalage kutoka Haki Elimu akichangia hoja wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022  uliofanyika leo Alhamis Juni 10,2021 katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.
Mdau Flora Mlowezi akichangia hoja wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Taifa mwaka 2021/2022  uliofanyika leo Alhamis Juni 10,2021 katika Ukumbi wa New Africa Hotel Jijini Dar es salaam.
Wadau wa haki za wanawake na jinsia wakipiga picha ya kumbukumbu

Wafanyakazi wa TGNP wakipiga picha ya kumbukumbu

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akifungua Mjadala wa hali ya uchumi mwaka 2020 (Kijiwe cha kahawa) katika Ukumbi wa TGNP Mabibo Jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi akizungumza wakati wa Mjadala wa hali ya uchumi mwaka 2020 (Kijiwe cha kahawa) katika Ukumbi wa TGNP Mabibo Jijini Dar es salaam.

Wadau wa haki za wanawake na jinsia wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa ya hali ya uchumi mwaka 2020 kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Mubashara kutoka Bungeni Dodoma kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba wakiwa katika Ukumbi wa TGNP Mabibo Jijini Dar es salaam.

Mkuu wa Programu TGNP , Shakila Mayumana akizungumza wakati wa Mjadala wa hali ya uchumi mwaka 2020 (Kijiwe cha kahawa) katika Ukumbi wa TGNP Mabibo Jijini Dar es salaam.

Afisa Habari TGNP akizungumza wakati wa mjadala huo
Afisa Programu Mwandamizi TGNP Anna Sangai akizungumza wakati wa mjadala huo
Renatus Rweyemamu akichangia hoja wakati wa mjadala huo
Afisa Programu Mwandamizi TGNP, Joyce Mkina akizungumza wakati wa mjadala huo

Mwanachama wa TGNP, Edward Mhina akichangia hoja wakati wa mjadala huo
Mdau Edes Joachim akichangia hoja ukumbini
Mdau Suzan Yumbe akichangia hoja ukumbini
Mdau Janeth John akichangia hoja ukumbini
Mdau William Baseka akichangia hoja ukumbini
Mdau Lydia Jacob akichangia hoja ukumbini
Mdau Salha Azizi akichangia hoja ukumbini
Mdau Tatu Ally akichangia hoja ukumbini
Wadau wa haki za wanawake na jinsia wakipiga picha ya kumbukumbu baada ya kufuatilia Mubashara uwasilishwaji wa taarifa ya hali ya uchumi mwaka 2020 kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Mubashara kutoka Bungeni Dodoma kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba wakiwa katika Ukumbi wa TGNP Mabibo Jijini Dar es salaam.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments