MWANAFUNZI AMCHOMA MSUMARI KICHWANI MWALIMU WAKE


Makachero kaunti ya Kericho nchini Kenya wanamsaka mwanafunzi wa kidato cha tatu aliyemshambulia mwalimu mkuu wake kwa kumchoma/kumshindilia msumari kichwani.

Mwanafunzi huyo ni wa shule ya upili ya Ainamoi na alimshambulia mwalimu mkuu baada ya kutakiwa kulipa karo. 

Kulingana na ripoti ya polisi, mwalimu mkuu alimtaka mwanafunzi huyo kulipa karo ya KSh 7000 lakini akaamua kuendelea msumari na kumchoma kichwani.

Mwanafunzi huyo alitakiwa  lakini akaendea msumari na kumjeruhi mwalimu mku
Kisa hicho kimezua wasiwasi katika shule ya upili ya Ainamoi kaunti ya Kericho huku kikosi cha waalimu kimesema kinahofia maisha yao na sasa wanataka serikali na wazazi kuwahakikishia usalama

Mwalimu huyo wa kiume alifikishwa hospitali kupata matibabu na hali yake imeelezwa kuwa salama sasa.

 Picha za mwalimu huyo akivuja damu kichwani baada ya msumari huo wa inchi nne kumuingia kichwani.

 Kisa hicho kimekashifiwa vikali na wazazi eneo hilo huku wanamtandao wakihoji kuhusu kizazi cha sasa cha wanafunzi.

Nickson Ekume alishangaa ni vipi mwanafunzi wa kidato cha tatu alipata ukakamavu wa kutekeleza mashambulizi hatari kama hayo.

 "Hili halikubaliki kabisa. Nahofia kuhusu kizazi ambacho kinakua kwa sasa kiasi cha kuwa wanaweza kushambulia waalimu wao," alisema Ekume.

"Hii ni ishara ya msongo wa mawazo ambao uko katika jamii yetu kwa sasa na linafaa kufanyiwa upekuzi zaidi kwa sababu mwanafunzi hawezi kumshambulia mwalimu tu vivi hivi," Geoffrey Kaira alisema.

Chanzo - Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments