WAZAZI WAMKATAA MKE WA KIJANA WAO...MWENYEWE AJILIPUA KWA PETROLI NA MKEWE

 

Mfano wa mlipuko wa petroli

Na Mwandishi wa Malunde 1 blog
Mwanaume aitwaye Wenslausi James (30) na Betha Kasimili (25), ambao ni wakazi wa kijiji cha Busongo kata ya Mwamashele wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga, wamefariki dunia baada ya mwanaume huyo kujilipua moto kwa kutumia mafuta ya Petroli, kwa madai ya wazazi wa mwanaume kumkataa mwanamke.

Kwa Mujibu wa Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga, Kamishina msaidizi wa Polisi, Jackson Mwakagonda,tukio hilo limetokea June 14 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi.

Amesema wanandoa hao walikuwa wamezaa watoto watatu, lakini wazazi wa mwanaume walimkataa mke wake, na kuamua kuuvunja mji pamoja na kurudisha mahari nyumbani kwao na mwanamke.

Aidha amesema baada ya mji huo kuvunjika, ndipo mwanaume akasikia kuwa mke wake anataka kuolewa, na kuamua kwenda kwao na mwanamke akiwa na dumu la mafuta ya Petroli lita tano,na kisha kuingia chumbani kwa mwanamke na kufunga mlango na kuanza kugombana.

"Mwanaume huyu alimchoma kisu cha ubavuni mke wake, na kisha kumfunga minyororo na kumwagia mafuta ya Petroli, kisha na yeye kujimwagia Petroli akawasha kiberiti na kujilipua moto, ambapo waliteketea pamoja na nyumba," amesema Mwakagonda.

Aidha Kamanda ametoa wito kwa wazazi, kuacha kuingilia ndoa za watoto wao, pamoja na wanandoa kuacha kujichukulia sheria Mkononi, na pale penye migogoro bali watafute ufumbuzi kwa kufuata sheria.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments