RC SHINYANGA DR. SENGATI, RAS MPYA BALOZI DR. BATILDA WAKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI..WAANIKA MIKAKATI KABAMBE

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Philemon Sengati na Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Buriani leo Jumatatu Juni 7,2021 wamekutana na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kwa ajili kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya mkoa wa Shinyanga ikiwa ni siku chache zimepita baada ya kuteuliwa kisha kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu kutekeleza majukumu yao mkoani Shinyanga.  Picha na Kadama Malunde & Frank Mshana
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Dkt. Philemon Sengati akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Juni 7,2021
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Dkt. Philemon Sengati akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Juni 7,2021
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Dkt. Balozi Batilda Salha Buriani akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Juni 7,2021
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Dkt. Balozi Batilda Salha Buriani akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Juni 7,2021
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakuru akizungumza kwenye kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Philemon Sengati na Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Buriani na waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Juni 7,2021
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Dkt. Philemon Sengati akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Juni 7,2021
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Dkt. Philemon Sengati akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Juni 7,2021
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Dkt. Philemon Sengati akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Juni 7,2021
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Dkt. Philemon Sengati akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Juni 7,2021
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Dkt. Philemon Sengati (mwenye suti ya Bluu katikati) akipiga picha ya pamoja na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Dkt. Philemon Sengati (mwenye suti ya Bluu katikati) akipiga picha ya pamoja na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Dkt. Philemon Sengati (mwenye suti ya Bluu katikati) akipiga picha ya pamoja na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde & Frank Mshana
****
Na Damian Masyenene, Shinyanga
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Philemon Sengati na Katibu Tawala wa mkoa huo, Balozi Dk. Batilda Buriani leo wamekutana na waandishi wa habari na kueleza mikakati yao katika kukuza uchumi wa mkoa huo, kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo na mipango kadhaa yenye lengo la kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi wake.

Viongozi hao ambao ni wapya kwa mkoa huo baada ya kuteuliwa hivi karibuni, Dk. Sengati akichukua nafasi ya aliyekuwa mkuu wa mkoa huo, Zainab Telack na Balozi Dk. Buriani akichukua nafasi ya Albert Msovela, wameeleza kuwa mkoa wa Shinyanga ni Tajiri kutokana na rasilimali ilizonazo lakini utajiri huo unapaswa kutafsiriwa kwa Maisha bora kwa wananchi, miundombinu Rafiki, elimu bora, upatikanaji sahihi wa dawa na uwekezaji.

Akizungumza kwenye kikao hicho, Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga, Balozi Dk. Batilda Buriani amesema kuwa wanafikria kubuni miradi mipya, kuanzisha kilimo cha mkataba cha Alzeti ili kuzalisha mafuta na kuondokana na changamoto ya uhaba wa mafuta nchini na kuboresha sekta ya mifugo na bidhaa zake ili iwe na tija.

Amesema mkoa huo unavyo vivutio vingi ikiwemo hifadhi ya Moyowosi-Kigosi na vingine ambavyo havijatangazwa ipasavyo, hivyo watatumia fursa hiyo kupanua wigo wa kupata mapato na uwekezaji nje ya vyanzo vilivyopo.

“Nimefarijika kuja hapa naona hali ya mazingira imebadilika siyo kame kama zamani na hali ya umaskini imepungua, tutapenda kuhakikisha utajiri na rasilimali vinaaksi hali ya maendeleo ya wananchi. Kwa pamoja tunataka kubadilisha sura na mwonekano wa Shinyanga, tunataka kutumia uzoefu wetu katika maeneo mbalimbali ili kuitangaza na kuipeleka nje Shinyanga na kuvutia uwekezaji.

“Tuna mengi lakini kubwa ni kuhakikisha tunaleta Chuo Kikuu na kukaribisha taasisi za kimataifa ili tuifanye Kahama kuwa Jiji. Kwenye afya tunataka kupunguza maambukizi ya Ukimwi, kuboresha hali ya upatikanaji wa dawa na huduma kwa Wazee, upatikanaji wa mikopo ya silimia 10 kwa akina mama, vijana na Walemavu kwenye halmashauri tutasimamia na kutengeneza miradi endelevu,” ameeleza.

Naye Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Philemon Sengati amesema kuwa Watanzania wakiwemo waandishi wa habari ni watu waadilifu na wenye nidhamu wanaolitakia taifa lao maendeleo na kwamba rasilimali za mkoa huo kwenye Madini, Mifugo, Kilimo na mkao wa biashara na uwekezaji vinaridhisha kwa kiasi kikubwa lakini vinatakiwa kuaksi utajiri huo na ubora wa maisha ya watu wake hasa walioko pembeni, hivyo hilo litakuwa kipaumbele cha mkoa kutafsiri huo utajiri katika maisha ya wana Shinyanga.

“Tunataka kupunguza Vifo vya akina amama, kuongeza kiwango cha elimu, uchumi wa mtu mmoja mmoja upande, miundombinu ijengwe kila mahali. Niombe Wanahabari mtupatie ushirikiano kwa pamoja tuweke kumbukumbu kwa watu wetu kwa kuweka alama chanya katika mkoa wetu,” amesisitiza.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC), Greyson Kakuru, amewashukuru viongozi hao kwa kuonyesha matumaini makubwa kwa waandishi wa habari, ambapo amewaomba kutengeneza mazingira Rafiki kwa Wanahabari katika kutangaza shughuli mbalimbali za mkoa huo.

Naye Mwakilishi wa Kituo cha Redio Faraja FM, Simeo Makoba, ameuomba uongozi wa mkoa huo kuwezesha upatikanaji wa taarifa kwa wakati sahihi katika idara mbalimbali kwa kuwashirikisha waandishi wa habari ili kufikia azma na malengo yaliyokusudiwa, huku akishauri vyombo vyote vya habari kushiriki kwenye ujenzi wa mkoa huo bila kubaguliwa kwa ukubwa ama udogo wake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments