BARRICK-NORTH MARA YATUNUKIWA TUZO KWA KUFANIKISHA UZINDUZI WA MWONGOZO WA UWEKEZAJI MKOANI MARA - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Tuesday, June 1, 2021

BARRICK-NORTH MARA YATUNUKIWA TUZO KWA KUFANIKISHA UZINDUZI WA MWONGOZO WA UWEKEZAJI MKOANI MARA


Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (Kulia) akikabidhi cheti kwa Meneja wa Mahusiano ya Jamii wa mgodi wa Barrick North Mara,Gilbert Mworia, (Kushoto) kutokana na mchango wa kampuni hiyo kufanikisha uzinduzi wa mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa Mara katika hafla iliyofanyika mjini Musoma. Katikati mwenye miwani ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, mhandisi Robert Gabriel Luhumbi.
Waziri Mkuu,Mhe. Kassim Majaliwa (Kulia) akikabidhi tuzo kwa Meneja wa Mahusiano ya jamii wa mgodi wa Barrick North Mara, Gilbert Mworia, (Kushoto) kutokana na mchango wa kampuni hiyo kufanikisha uzinduzi wa mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Mara, katika hafla iliyofanyika jana mjini Musoma.Katikati mwenye miwani ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, mhandisi Robert Gabriel Luhumbi.
Kampuni ya Barrick ilishiriki pia katika maonyesho hayo

***

Kampuni ya Barrick, kupitia mgodi wake wa North Mara, imetunukiwa tuzo kwa  kufanikisha uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji (Investment Guide ) mkoani Mara uliofanyika katika viwanja vya Mwembeni Complex,  mjini Musoma ambapo mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhshimiwa Kassim Majaliwa.

Mhe. Kassim Majaliwa, alitumia nafasi hiyo ya kuzindua mwongozo kwa kuwakaribisha wawekezaji kuchangamia fursa mbalimbali za uwekezaji  mkoani humo na kuwahakikishia kuwa Serikali ya awamu ya 6 itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchi ma kuondoa vikwazo vinavyozorotesha  uwekezaji.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mara, Mhandisi Robert Gabriel ,alishukuru wadau mbalimbali waliofanikisha maandalizi ya uzinduzi huo  ikiwemo kampuni ya Barrick kupitia mgodi wake wa North Mara.

Kwa kutambua mchango huo kampuni Waziri  Mkuu,Mh.Kassim Majaliwa ilkabidhiwa tuzo na cheti   kwa watendaji wa mgodi wa Barrick North Mara.

Mbali na kufanikisha  uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji, Barrick imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali kuboresha uchumi wa kijamii ikiwemo kukabiliana na changamoto mbalimmbali za kijamii hususani katika sehemu zinazozunguka maeneo yake ya kazi.

Mchakato wa Serikali kuanzisha mpango wa kila mkoa kuzindua Mwongozi wa uwekezaji umelenga kuonyesha fursa za uwekezaji zilizopo katika maeneo,ili kuvutia wewekezaji wa nje,kukuza biashara katika mikoa hiyo hayo  na kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii.

Uzinduzi huo umekuwa ukifanyika sambamba na maonyesho ya bidhaa ya wajasiriamali na makampuni  kwa ajili ya kutagaza biashara na shughuli zao mbalimbali.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages