WAZIRI LUKUVI AZITAKA TAASISI ZA SERIKALI KUTENGA BAJETI YA FIDIA KABLA YA KUTWAA MAENEO - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Wednesday, May 26, 2021

WAZIRI LUKUVI AZITAKA TAASISI ZA SERIKALI KUTENGA BAJETI YA FIDIA KABLA YA KUTWAA MAENEO


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amezitaka wizara, taasisi na mamlaka mbalimbali kuhakikisha zinatenga bajeti kwa ajili ya kulipa fidia kabla ya kutwaa ardhi kutoka kwa wananchi.

Lukuvi ameyasema hayo leo Jumatano Mei 26,2021 wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2021/22.

Amesema jumla ya migogoro ya ardhi 3,171 ilipokelewa kupitia programu ya Funguka kwa Waziri ambapo hadi kufikia  Mei 15,  2021 migogoro 1,144 ilishughulikiwa.

Amebainisha kuwa kati ya migogoro hiyo asilimia 39 inahusu masuala ya fidia.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages