TAKUKURU MPWAPWA YAFANIKIWA KUMREJESHEA TSH. MILIONI 2.4 MZEE MSTAAFU ALIZOPIGWA MIKOPO UMIZA

 Mkuu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa[TAKUKURU]Wilaya ya Mpwapwa   Bi. Julieth Mtui   akimkabidhi fedha kiasi cha Tsh.Milioni mbili ,laki nne na sabini na tano elfu[ 2,475,000/= ] mzee mstaafu Benedict   Mtihani  alizodhurumiwa  kutoka kwenye sehemu ya  fedha zake za kiinua mgongo na kijana  mmoja aliyekuwa  akijihusisha na ukopeshaji wilayani humo.

***

Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma

Taasisi ya   Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania [TAKUKURU]Wilaya ya  Mpwapwa    imefanikiwa  kurejesha kiasi cha Tsh.milioni   mbili ,laki nne na sabini na tano elfu [. 2,475,000/= ] kwa mzee mstaafu Benedict   Mtihani  alizodhurumiwa  kutoka kwenye fedha zake za kiinua mgongo na kijana  mmoja aliyekuwa  akijihusisha na ukopeshaji wilayani humo bila kufuata utaratibu.

Akizungumza na  na Mtandao huu ,Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya  Mpwapwa  Julieth Mtui  amesema ofisi ya TAKUKURU  Mpwapwa  ilipokea taarifa kutoka kwa mzee mmoja mstaafu katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mpwapwa  masuala ya ulinzi alikopa kwa kijana anayejihusisha na mikopo umiza na baada ya fedha za kiinua mgogo  kutoka kijana yule alimkata zaidi ya Tsh.milioni 11  kwenye akaunti ya benki kwani alikuwa ameshamnyang’anya kadi ya benki.

Mkuu  huyo wa TAKUKURU ameendelea kufafanua kuwa,katika uchunguzi waliofanya walibaini kuwa fedha alizopaswa kulipa mzee ni  pamoja  na riba  ni Tsh.Milioni nane  laki mbili na elfu hamsini [8,250,000 ].

Hata hivyo mkuu huyo wa TAKUKURU ametoa ushauri kwa wastaafu na wanaotarajia kustaafu  kujitahidi kwenda kwenye Taasisi zinazotambulika kisheria na kuwa na uelewa zaidi juu ya masuala ya riba na uhalali wa wakopeshaji hao.

Kwa upande wake Mzee Mstaafu  Benedict Mtihani ameelezea jinsi alivyotapeliwa fedha za kiiunua mgongo huku akiipongeza TAKUKURU kwa kuweza kuokoa pesa zake.

“Kwa kweli nashukuru sana TAKUKURU kwa kuweza kunisaidia kuokoa fedha zangu ,niliambiwa na huyo kijana kuwa riba ya mkopo ni nzuri lakini nilinyang’anywa kadi ya benki baada ya mafao ya kiinua mgongo kutoka kakomba fedha zote kwenye akaunti”amesema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments