KOM GROUP OF COMPANIES LTD YAKABIDHIWA NYARAKA ZA UMILIKI ENEO LA KIWANDA CHA KUCHAKATA NYAMA ZA KUKU, CHAKULA CHA MIFUGO PWANI

Kampuni ya KOM Group Of Companies Limited ya Mjini Kahama mkoani Shinyanga leo Jumatatu Mei 10,2021 imekabidhiwa nyaraka za kumiliki eneo la heka 100 kwa ajili ya uwekezaji wa Kiwanda cha kuchakata nyama za kuku na chakula cha mifugo katika eneo la Kibaha vijijini mkoani Pwani. Kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akikabidhi nyaraka hizo leo jijini Dodoma kwa Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya KOM Group Of Companies Limited Shija Felician (kulia).
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya KOM Group Of Companies Limited Shija Felician (kulia) akionesha nyaraka za kumiliki eneo la heka 100 kwa ajili ya uwekezaji wa Kiwanda cha kuchakata nyama za kuku na chakula cha mifugo katika eneo la Kibaha vijijini mkoani Pwani. Kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments