KAMPUNI YATANGAZA NAFASI ZA KAZI ZA KULALA

Kampuni moja nchini Marekani ambayo hutoa vidokezo vya usingizi imetangaza nafasi za kazi ya weledi wa usingizi sawa na takribani shilingi Milioni 3.3. za Tanzania.

Kampuni ya Eachnight imesema inawatafuta watu wa kujiunga na kikosi cha utafiti kama weledi wa kulala kubaini umuhimu wa usingizi na hasara yake. 

"Kwa sasa tunaajiri kikosi cha watu watano ambao watakuwa weledi wa usingizi na kulipwa kulala! Pia hatufanyi matani," ilisema kampuni hiyo kwenye tovuti yake. 

Kampuni hiyo iliwaomba wale ambao wangelipenda kuwa sehemu ya utafiti huo kuwasilisha maombi yao mtandaoni kabla ya Mei 31, 2021. 

Watakaofaulu kupata kazi hiyo watalipwa KSh 159,000 na wataanza punde baada ya kuchaguliwa kwa kipindi cha siku 30 za utafiti huo. Watakaotuma maombi ni lazima walale pekee yao wakati wa kipindi hicho ili kuhakikisha kuwa usingizi wao haukatizwi.

Wakati wa utafiti huo, watafiti watabaini muda mwafaka wa kulala na athari za kulala sana hadi kuchoka. 

Mambo mengi watakayozingatia ni athari za usingizi kwa kumbukumbu, motisha na tija Kama sehemu ya utafiti na kufaulu kwake, kutakuwa na simu za video baada na wakati wa utafiti na kuulizwa maswali ya moja kwa moja ambapo weledi wa usingizi wataelezea ushuhuda wao.

CHANZO - TUKO NEWS


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments