Picha : RAIS SAMIA AZINDUA KITABU CHA HISTORIA YA MAISHA YA RAIS MSTAAFU MZEE ALI HASSAN MWINYI...AMKABIDHI GARI JIPYA | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, May 8, 2021

Picha : RAIS SAMIA AZINDUA KITABU CHA HISTORIA YA MAISHA YA RAIS MSTAAFU MZEE ALI HASSAN MWINYI...AMKABIDHI GARI JIPYA

  Malunde       Saturday, May 8, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akinyanyua juu Kitabu cha Historia ya Maisha ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi mara baada ya kukizindua katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Convention Centre Jijini Dar es Salaam leo tarehe 08 Mei, 2021.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikata utepe ili kuzindua Kitabu cha Historia ya Maisha ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Convention Centre Jijini Dar es Salaam leo tarehe 08 Mei, 2021.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi akinyanyua juu Kitabu cha Historia ya Maisha yake mara baada ya kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Gari Jipya Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi pamoja na Mkewe Mama Sitti Mwinyi mara baada ya kuzindua Kitabu chake cha Historia ya Maisha yake ili liweze kumsaidia katika shughuli mbalimbali za usafiri.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi akizungumza na viongozi mbalimbali waliofika katika uzinduzi wa Kitabu chake cha Historia ya Maisha yake katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Convention Centre.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Maisha ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi iliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Convention Centre.

PICHA NA IKULU
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post