MWANAMKE AZUA GUMZO KUWEKA NYOKA KWENYE JENEZA LA MME WAKE


Mwanamke mmoja kutoka Ghana amezua hisia mseto kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana kwenye video akiweka nyoka ndani ya jeneza la mumewe.

Iliripotiwa kuwa mwanamke huwa alikuwa ameghadhabishwa na waliohusika na kifo cha mumewe na alitaka wapate adhabu kali.

Kwenye video hiyo ambayo imesambaa mitandaoni, mwanamke huyo alidai kwamba mumewe aliuawa kwa kuumwa na nyoka kwenye ulimi na anaamini kuna watu walipanga njama hiyo.

 Ilisemekana kwamba jamaa huyo aliuawa kwa kuumwa na nyoka kwenye ulimi kwa hivyo mkewe akamua kumzika nayo ambapo kulingana na mila, mwanamke huyo alifanya hivyo ili nyoka huyo akabiliane na wale waliohusika na kifo cha mumewe 

Video hiyo iliibua hisia tofauti miongoni mwa wanamitandao  baadhi ya maoni;

 @funghana_ Alisema inaaminika kwamba jamaa huyo aliuawa, kwa hivyo nia yake kuwekewa nyoka ilikuwa ni kukabiliana na waliohusika na kifo chake.

 @bby__naa." Naye alisema .“Hii ni kama kukiuka haki za nyoka , wao pia wana haki zao”

 @cabi_diana: “Haya ni maajabu.

” @wurdzfreeman “Ati aliumwa na nyoka kwa ulimi? kivipi na inawezakanaje?”

 @ericaabyna: “Eish, hii inamaanisha nini?”

 @jerryjustice: “Aaah, Hii ni nini sasa?” 

@1plus1builders: “Hii ni muvi ama nini?”

TAZAMA HAPA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments