Picha : DC MACHA AONGOZA MAADHIMISHO SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI SHINYANGA....ATAKA VISHOKA WA HABARI WADHIBITIWE

Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akizungumza leo Jumatatu Mei 3,2021 wakati wa Maadhimisho siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Mkoa wa Shinyanga  yaliyofanyika katika Manispaa ya Kahama

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha amewataka waandishi wa habari kuilinda tasnia ya habari kwa kuhakikisha wanawaondoa waandishi wa habari vishoka ‘makanjanja’ ambao wamekuwa wakiharibu taswira ya tasnia hiyo kwa kuandika na kusambaza habari za uongo ‘Fake News’.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Mei 3,2021 wakati wa Maadhimisho siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Mkoa wa Shinyanga  yaliyofanyika katika Manispaa ya Kahama yakiongozwa na kauli mbiu ni ‘Habari kwa Manufaa ya Umma’ yaliyoandaliwa na Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC) na kuhudhuriwa na wadau wa habari mkoa wa Shinyanga.

“Tasnia ya Habari sasa imeingiliwa, na inataka kuonekana haiheshimiki. Ndani yenu wamo vishoka wanaandika na kusambaza taarifa ambazo siyo sahihi na wenye jukumu la kuilinda tasnia hii ya habari ni nyinyi waandishi wa habari.

 Pamoja na uhuru uliopo lakini na nyinyi tunaomba mtusaidie kuwaondoa vishoka katika tasnia ya habari maana kila wakati tunaona habari za uongo 'Fake News'. Sisi kama serikali tupo tayari kushirikiana nanyi kuwabaini vishoka”,amesema Macha.

“Tusikubali watu wasio na uelewa na masuala ya uandishi wa habari wavamie tasnia hii. Ili kujenga heshima ya taaluma ya habari wilayani Kahama naomba nipewe orodha ya waandishi wa habari waliopo Kahama na mkoa wa Shinyanga kwa ujumla ili mwandishi anapofika ofisini kwangu nijue kama taarifa tunazotoa zinatolewa kwa mwandishi sahihi”,ameongeza Macha.

Macha amewasisita waandishi wa habari kuandika habari sahihi kwa manufaa ya umma huku akivisihi vyombo vya habari kuandika habari za uchunguzi badala ya kutoa tu taarifa.

“Vyombo vya habari vina fursa ya kuchangia masuala mbalimbali yanayohusu jamii, tunachokiomba tuwe na uandishi unaojenga, uandishi wenye staha. Na nyie waandishi wa habari andikeni mazuri tunayofanya, andikeni ya kutukosoa, andikeni kwa staha, habari ilenge kufundisha, kutoa taarifa na hakikisheni uandishi wenu unakuwa wa kizalendo,kulinda nchi  na wa staha”,amesema Macha.

Pia amezitaka taasisi za umma kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari zitambue vyombo vya habari vilivyopo katika maeneo yao na kutoa taarifa mbalimbali ili kuepusha waandishi wa habari kuandika taarifa zisizo sahihi kwani wakati mwingine wanapokosa ushirikiano waandika taarifa wanazoziona ambazo wakati mwingine zinakuwa siyo sahihi.

Aidha amewataka waandishi wa habari kuendelea kutoa taarifa kwa kujiridhisha kwa pande zote mbili na wazingatie kuandika habari kwa usahihi na kutoyaacha nyuma masuala ya kiuchumi.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akizungumza leo Jumatatu Mei 3,2021 wakati wa Maadhimisho siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Mkoa wa Shinyanga  yaliyofanyika katika Manispaa ya Kahama
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akizungumza leo Jumatatu Mei 3,2021 wakati wa Maadhimisho siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Mkoa wa Shinyanga  yaliyofanyika katika Manispaa ya Kahama
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru akizungumza leo Jumatatu Mei 3,2021 wakati wa Maadhimisho siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Mkoa wa Shinyanga  yaliyofanyika katika Manispaa ya Kahama

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akizungumza wakati wa Maadhimisho siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Mkoa wa Shinyanga  yaliyofanyika katika Manispaa ya Kahama
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga Patrick Mabula akizungumza leo Jumatatu Mei 3,2021 wakati wa Maadhimisho siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Mkoa wa Shinyanga  yaliyofanyika katika Manispaa ya Kahama

Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akipiga picha ya pamoja na wadau wa habari wakati wa Maadhimisho siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Mkoa wa Shinyanga  yaliyofanyika katika Manispaa ya Kahama leo Mei 3,2021
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akipiga picha ya pamoja na waandishi wa habari na wadau wa habari wakati wa Maadhimisho siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Mkoa wa Shinyanga  yaliyofanyika katika Manispaa ya Kahama leo Mei 3,2021

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments